Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima zake za mwisho kwa mwili wa
Marehemu Dkt William Shija alipoongoza shughuli za kuaga leo Jumapili
Oktoba 12, 2014 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimpa pole Mama Getrude Shija, Mjane wa Marehemu
Dkt William Shija alipoongoza shughuli za kuaga leo Jumapili Oktoba 12,
2014 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi kitabu cha maombolezo cha msiba wa
Marehemu Dkt William Shija alipoongoza shughuli za kuaga leo Jumapili
Oktoba 12, 2014 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akimwelekeza jambo ofisa wa Bunge wakati wa
shughuli za kutoa heshimam za mwisho kwa Marehemu Dkt William Shija
alipoongoza shughuli za kuaga leo Jumapili Oktoba 12, 2014 katika
viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam
Bw.
Saidi Yakubu, MC wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu Dkt
William Shija leo Jumapili Oktoba 12, 2014 katika viwanja vya Karimjee
jijini Dar es salaam
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Anne Makinga akiongea
wakati wa shughuli za kuaga mwili wa marehemu Dkt William Shija leo
Jumapili Oktoba 12, 2014 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es
salaam
Sehemu ya waombolezaji
Rais
Kikwete akipeana mikono na Kaimu Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya
Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA) baada ya kutoa salamu za rambirambi
kutoka makao makuu ya CPA jijini London.
Kaimu
Katibu Mkuu wa Chama cha Mabunge ya Nchi za Jumuiya ya Madola (CPA)
akimkabidhi binti wa marehemu vitabu vya maombolezo vilivyotiwa saini na
waombolezaji huko London Uingereza.
Familia
ya marehemu Dkt William Shija wakiwa katika shughuli za kuaga mwili
leo Jumapili Oktoba 12, 2014 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es
salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo,
Jumapili, Oktoba 12, 2014, ameungana na waombolezaji kutoa heshima za
mwisho na kuaga mwili wa Katibu Mkuu wa Kwanza Mwafrika wa Chama cha Mabunge ya
Jumuia ya Madola (CPA) Dkt. William Ferdinand Shija, ambaye pia alipata kuwa
Waziri Mwandamizi wa Serikali, katika shughuli iliyofanyika kwenye
Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam.
Rais
Kikwete amewasili kwenye Viwanja vya Karimjee kiasi cha saa 4:10 asubuhi
kujiunga na Makamu wa Rais, Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Mwenyekiti wa
CPA-Kanda ya Afrika Mheshimiwa Anne Makinda ambaye pia ni Spika wa Bunge la Tanzania,
viongozi na wananchi kutoa heshima za mwisho.
Baada
ya kuaga mwili, Rais Kikwete ametia saini Kitabu cha Maombolezo ya Dkt. Shija
ambaye alifariki dunia Jumamosi ya wiki iliyopita, Oktoba 4, 2014 kwenye
Hospitali ya Charing Cross mjini London, Uingereza ambako alikuwa anapata
matibabu ya ugonjwa wa Saratani. Makazi yake ya kazi yalikuwa huko huko
Uingereza.
Miongoni
mwa waombolezaji wengi kwenye shughuli hiyo ya leo ulikuwa ni ujumbe mzito wa
CPA ukiongozwa na Mwenyekiti wake, Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Lindiwe Maseko
wa Afrika Kusini. Pia shughuli hiyo imehudhuriwa na Bwana Joe Omoldin ambaye
sasa ni Kaimu Katibu Mkuu wa Chama hicho.
Dkt.
Shija ambaye alizaliwa katika Kijiji cha Nyalukomba, Wilaya ya Sengerema, Mkoa
wa Mwanza, Aprili 28, Mwaka 1947, alipata elimu ya awali maeneo ya kwako kabla
ya kujiunga na Sekondari ya Chopra mjini Mwanza kwa elimu ya sekondari na
kuhitimu ualimu katika Chuo cha Ualimu cha Chan’gombe cha Dar es Salaam Mwaka
1968.
Baadaye,
Dkt. Shija alipata Shahada ya kwanza ya Uzamili ya Uandishi wa Habari nchini
India kabla ya kupata Shahada ya Uzamivu ya fani hiyo hiyo ya Uandishi wa
Habari katika Chuo Kikuu cha Howard cha mjini Washington, D.C., Marekani. Wakati
wote wa masomo yake alikuwa Mhadhiri wa Uandishi kwenye Chuo cha Nyegezi,
Mwanza.
Dkt.
Shija aligombea na kushinda Ubunge wa Jimbo la Sengerema Mwaka 1990 na kuingia
Serikali ambako alishikilia nafasi tofauti kwa vipindi tofauti kama
Waziri wa Elimu ya Juu, Sayansi na Teknolojia, Waziri wa Habari na Utangazaji,
Waziri wa Nishati na Madini na Waziri wa Biashara na Viwanda. Dkt. Shija pia amepata kuwa Mkuu wa Mkoa wa
Mwanza.
Katika
Mkutano Mkuu wake wa 52, Desemba, Mwaka 2006 mjini Abuja, Nigeria, Dkt. Shija
alichaguliwa, baada ya mchuano mkali sana, kuwa Katibu Mkuu wa Kwanza
Mwafrika wa CPA, taasisi ambayo tokea kuanzishwa kwake Mwaka 1911 ilikuwa
haijapata kumchagua Mwafrika kuwa Mtendaji Mkuu wake.
Alichaguliwa
kwa kipindi cha pili Mwaka 2012 baada ya kumaliza kipindi chake cha kwanza cha
miaka mitano. Alikuwa anamaliza muda wake Desemba 2016.
Mpaka
anaaga dunia, Dkt. Shija alikuwa ameshikilia nafasi ya Ukatibu Mkuu wa CPA kwa
mafanikio makubwa sana kwa miezi saba na miezi tisa. Atazikwa kesho, Jumatatu,
Oktoba 13, 2014 katika kijiji cha kwao cha Nyalukomba, Sengerema, Mwanza.
Imetolewa na;
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es
Salaam.
12
Oktoba,2014
Post a Comment