Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsifia Mbunge wa Jimbo la Isimani,
William Lukuvi kwa uchapakazi wake mzuri wakati wa mkutano wa hadhara
uliofanyika katika Kijiji cha Magozi, Kata ya Ilolo Mpya, Iringa Vijini
leo. Kinana alimjia juu Waziri wa Maliasili na Utalii, Nyalandu kwa
kushindwa kutafutia ufumbuzi migogoro ya wananchi.Pia aliwataka wananchi
kuacha kukwepa majukumu yao ya kuwatumikia Wananchi. PICHA ZOTE NA
RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye akihutubia katika mkutano huo
Kinana akisalimiana na wananchi alipowasili kushiriki ujenzi wa jengo la CCM tawi la Luganga Kata ya Ilolo Mpya.
Katibu
Mkuu wa CCM, Komredi Kinana na Mbunge wa Jimbo la Isimani, William
Lukuvi wakishiriki kufyatua tofali za ujenzi wa jengo la Ofisi ya CC,
Kinana na Lukuvi wakisaidia kufyatua tofali za kujengea jengo hilo la CCM
Wanachama
wa CCM Shina namba 6 katika Kijiji cha Magozi, Kata ya Ilolo Mpya
wakicheza kwa furaha wakati Kinna alipofika kuzungumza nao
Kinana akizungumza na wananchama wa shina hilo. Kulia kwake ni Balozi wa shina hilo Chengula Mlula
Kinana na Lukuvi wakitoka kukagua ujenzi wa Zahanati ya Magozi Kata ya Ilolo Mpya, Isimani
Kinana na Lukuvi wakijadiliana jambo baada ya kukagua ujenzi huo
Wamasai wakiingia kwenye mkutano kutumbiza kwa ngoma ya asili
Wasanii wakicheza ngoma ya asili ya kabila la wasukuma
Lukuvi
akimkabidhi kompyuta na mashine ya kudurufia Mwalimu Mkuu wa Shule ya
Sekondari Pawaga Charles Mgimwa kwa ajili ya matumizi ya shule
Mgimwa akifurahia msaada huo
Katibu
wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini, Amina Imbo (kushoto) akijadiliana
jambo na Mwenyekiti wa UWT wa wilaya hiyo, Shakila Kiwanga wakati wa
mkutano huo
Mbunge
wa Jimbo la Isimani, ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,
(Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi akielezea miradi
inayyotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya CCM jimboni humo.
Mmoja wa wananchi akiuliza swali kwa Katibu Mkuu Kinana kuhusu mgogoro wa ardhi wa wanakijiji na Jeshi la Magereza.
Mkuu
wa Mkoa wa Iringa, Ishengoma akijibu swali hilo ambapo alisema kuwa kwa
asilimia kubwa wamelitafutia ufumbuzi na kwamba kilichobaki ni wizara
husika kwenda kupima na kuweka alama za mipaka.
Post a Comment