Waokoaji
wakijindaa kwenda katika eneo ilipotokea ajali ya mitumbwi iliyobeba
harusi kutoka Kigoma mjini kwenda katika kijiji cha Kigalya kutafuta
miili ya marehemu ambayo bado haijapatikana
Ndugu, jamaa na wapambe wa bwana na bibi harusi walionusurika katika ajali ya mtumbwi katika kijiji cha Kalalangabo wakiwa wanaendelea na matibabu katika hospita ya Mkoa wa Kigoma |
Na Editha Karlo wa
Globu ya Jamii, Kigoma
WATU sita wamekufa maji katika ziwa Tanganyika na wengine 11 kunusurika kifo akiwemo bwana harusi Shaaban Idd na bibi harusi
Tukio
hilo limetokea leo saa nane na nusu mchana baada ya mitumbwi hiyo
kupigwa wimbi kali na kuzama katika kijiji cha Kalalangabo wakati bwana
harusi huyo akitoka kuoa katika eneo la mwandiga na kurudi nyumbani
akiwa na ndugu na jamaa pamoja na wapambe.
Akiongea
na Globu ya Jamii katika wodi namba 5 katika Hospital ya Mkoa wa
Kigoma alipolazwa bibi harusi huyo alisema kuwa alishikwa na bumbuwazi
sana baada ya tukio hilo kwani mpaka sasa bado hajielewi.
''Sikumbuki kitu kwani baada ya mtumbwi kuzama kila mtu alikuwa anahangaika kujiokoa na kifo.
"kwakweli
mimi naona kama mkosi siku ya harusi yangu watu wanakufa ila namshukuru
Mungu kwa kutunusuru na kifo na yote mimi nimemwachia Mungu''alisema
bibi harusi huyo
Mwathirika
mwingine aliyenusurika katika ajali hiyo Zabibu Issa alisema kuwa
mitumbwi waliyokuwa wamepanda ilikuwa imejaza sana watu na mizigo ndiyo
maana ilizidiwa uzito na kuzama baada ya kupigwa na wimbi.
''Safari
ya kwenda kijijini kwetu lazima tupite njia za majini hakuna barabra
kabisa sababu vijiji tunavyoishi vipo mwambao mwa ziwa Tanganyika
kungekuwa na barabara tungepita barabrani''alisema Bi Zabibu Issa.
Naye
muuguzi wa wodi namba tano walipolazwa majeruhi hao alisema kuwa
majeruhi wote waliopo wodini hali zao zinaendelea vizuri na kwamba mpaka
sasa wameshapokea jumla ya maiti sita.
Kamanda
wa polisi wa Mkoa wa Kigoma Jafari Mohamed akithibitisha hayo alisema
kuwa mpaka sasa jumla ya watu 27 wameshaokolewa, na miili sita kuopolewa
pamoja na walionusurika 11.
"Lakini
bado inahofiwa kuwa kuna miili mingine zaidi ambao bado haijapatikana
kwani mitumbwi hiyo inakadiriwa kuwa ilikuwa na watu zaidi ya sabini",
alisema na kuongezea kuwa vikosi vya ukoaji kwa kushirikiana na askari
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania vinaendelea na kazi ikiwa ni sambamba
na kuchunguza chanzo cha tukio hilo.
Post a Comment