Msanii maarufu wa filamu nchini King Majuto amesema kuwa ana nia ya kufanya filamu ya pamoja na Wema Sepetu na Diamond Platnumz.
Akizungumza na Bongo5, King Majuto ambaye filamu zake nyingi zinafanya vizuri sokoni alisema kuwa amekutana na Wema hivi majuzi na kumueleza hilo na kumtaka azungumze kuhusu project hiyo ili Diamond akikubali wafanye kazi pamoja.
Majuto alisema kuwa sio kwamba yeye ameshindwa kuzungumza na Diamond bali kwasababu ameanza kukutana na Wema ndiyo akamweleza kwanza.
"Hivi karibuni nilikuwa na Wema, nimemwamia aongee na Diamond ili tufanye filamu ya pamoja mimi Wema na Diamond, hata Diamond ninawe kuzungumza nae sema nimeanza na Wema Kwanza, akikubali mtasikia tu" alisema King Majuto ambapo pia alisema ili kucheza filamu ya mtu ni lazima alipwe mil.3 cash.
Ingawa uwezo wa Diamond katika filamu bado haujulikani lakini kama mastaa hao wote watu wakiwa ndani ya filamu moja na kupata msambazaji mzuri na mkweli ni lazima wafaidike kwa mauzo makubwa ya filamu hiyo.
Post a Comment