Manchester
United msimu huu imejaribu kujiimarisha katika idara ya ushambuliaji
kwa kufanya usajili wa kuvunja rekodi nchini Uingereza wakiwa na nia ya
kutaka kurejesha makali yao yaliyopotea msimu uliopita lakini uwepo wa
majeruhi takribani tisa ndani ya kikosi cha mashetani wekundu hao
kinaifanya klabu hiyo kuweweseka.
Hivi
karibuni klabu hiyo imetokea kumuamini mlinzi kinda Paddy McNair
aliyekuwa akishirikiana vyema na Muajentina Marcos Rojo katika
kuimalisha ulinzi wa katikati wa klabu hiyo lakini katika kile
kinachoonekana kama kuandamwa na jinamizi la mkosi wa majeruhi kijana
huyu naye amelipotiwa kupata maumivu ya misuli daraja la tatu
aliyoyapata siku ya Jumapili wakati timu yake ya Manchester United
ilipokipiga dhidi ya Everton na kupata ushindi wa magoli 2:1.
Kuumia
kwa McNair kunatimiza idadi ya walinzi watano wa wa klabu ya Manchester
United wanaokaa nje ya uwanja kutokana na majeruhi ambapo wengine ni
Luke Shaw (kifundo cha mguu), Jonny Evans (kifundo cha mguu), Phil Jones
(misuli) na Chris Smalling (nyama za paja).
Wachezaji
Ander Herrera (mbavu), Jesse Lingard (kifundo cha mguu), Michael
Carrick (mguu) na Ashley Young (nyonga) nao wanaungana na walinzi hao
watano katika orodha ya majeruhi ndani ya United wakati Wayne Rooney
anaendelea kutumikia adhabu yake ya kadi nyekundu aliyoipata kwenye
mchezo dhidi ya West Ham.
Wakati
Manchester United ikiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya majeruhi,
Arsenal wao wanashika nafasi ya pili katika orodha hiyo na kibaya zaidi
ni kuwa idadi kubwa ya wachezaji walio majeruhi kwenye kikosi cha
Mfaransa Wenger ni wale wa kikosi cha kwanza.
Mikel
Arteta, Aaron Ramsey, Mathieu Debuchy, Olivier Giroud na Theo Walcott
ni miongoni mwa wachezaji majeruhi wa klabu ya Arsenal na wengi wao ni
wachezaji wa kikosi cha kwanza cha timu hiyo.
Ifuatayo ni orodha ta majeruhi katika vilabu mbali mbali vya EPL mpaka hivi leo:
ORODHA YA WACHEZAJI MAJERUHI KWA VILABU VYA PREMIER LEAGUE KWA MSIMU WA 2014/2015.
Manchester United -9
Arsenal- 7
Burnley -7
Everton -7
Newcastle -7
West Ham -7
Liverpool- 6
Southampton- 5
Chelsea -4
Stoke City- 4
Swansea City- 4
Aston Villa- 3
Hull City -3
Sunderland- 3
West Brom -3
Crystal Palace- 2
Leicester City- 2
Manchester City -2
Queens Park Rangers- 2
Post a Comment