Nakala
ya Hati ya Kusafiria ya Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu ambapo
inaonyesha ana miaka 25 sasa Aliyesema ana miaka 18, 23
tumueleweje?PICHA KWA HISANI YA JAMII FORUMS.
Hii ni
nakala ya Leseni ya Udereva ya Miss Tz 2014 ambayo inaonyesha amezaliwa
31/5/1989 sasa hapa mbona kuna mkanganyiko yupi anasema ukweli?
Nakala
ya Cheti halisi cha Kuzaliwa cha Miss Tz 2014 Sitti Mtemvu kikionyeshwa
leo wakati kamati ya Miss Tz ilipokutana na wanahabari kwaajili ya
Kuzungumzia swala la Umri wa Miss Tz 2014
Baada
ya maneno mengi kuzungumzwa na wadau wa maswala ya Urembo Nchini na
kuandikwa sana kwenye Mitandao ya Kijamii ambapo headline ilikua ni Umri
wa Miss Tz 2014 leo Kamati ya Miss Tz ikiongozwa na Bosi wao Hashim
Lundenga wahitisha mkutano na waandishi wa Habari kwa kwaajili ya
kuzungumzia Umri sahihi wa Miss Tz 2014 na kuamua kuonyesha cheti chake
cha Kuzaliwa Mbele ya Waandishi wa habari.
Mara
baada ya Kuonyeshwa kwa cheti cha Kuzaliwa cha Miss Tz 2014 mapya
yaibuka ambapo watu mbalimbali nchini wamekuwa wakijiuliza je zile
nayaraka zilizokuwa zikionyeshwa katika Mitandao ya Kijamii sio zake au
je Walikosea?
Sasa
tujiulize swali Dogo tu...Tumeona cheti ndio lakini cheti hiko sawa
hatukatai kwa hilo lakini Je Zile nyaraka zilizozagaa kama hati yake ya
Kusafiria ambayo imeonyesha kazaliwa Mwaka 31/05/1989 ilikosewa? Sio
yake? au Mamlaka husika ambayo ni Uhamiaji Walifoji na ili iweje? Hapa
ndipo inapotupa shaka kuendelea kuamini kamati ya Miss Tz kwasababu sio
hati ya Kusafiria tu Je Vipi Kuhusu Leseni yake ya Udereva ya Huko Texas
Nchini Marekani nayo si yake? au nayo Wamekosea?
Napata
Shida kufahamu na kuelewa kwanini hili limetokea hivi kwa Maana Umri
wake Upo kwenye nyaraka Muhimu sana Ambazo naamini Kabisa Uhamiaji
hawawezi kukosea kirahisi katika umri wa mtu na Vilevile leseni ya
Udereva nayo Ya Huko Marekani nayo ya Magumashi au?
Kipi
kieleweke hapa Maana Cheti kilichoonyeshwa leo kinaonyesha ana Miaka 23
ambapo amezaliwa 31 May 1991 na Nyaraka hizo hapo Juu Kuanzia Hati yake
ya Kusafiria inaonyesha Amezaliwa tarehe 31 May 1989 sasa kipi ni kipi
maana hata leseni yake ya Udereva ya Huko Marekani inaonyesha inaonyesha
amezaliwa tarehe 31 May 1989 sasa hapa bado Hakijaeleweka....
Kazi Kweli Kweli.....
Post a Comment