Wasanii wa Wanaume Family, kutoka kushoto, Dogo Aslay, Stiko na Yesaya Ambilikile YP (kulia) wakiwa katika pozi.
Msanii
wa kundi la TMK Wanaume Family,Yesaya Ambilikile ‘ Y- P’ amefariki
dunia usiku wa leo katika Hospitali ya Temeke baada ya kusumbuliwa kwa
muda mrefu na ugonjwa wa kifua.
Akizungumza
na mtandao huu Kiongozi wa kundi hilo, Said Fela, amethibitisha msiba
huo na kusema ratiba kamili itatoka leo mchana.
“Mpaka
sasa hivi bado hatujaandaa ratiba, tunasubirika kaka yake kwa sababu
huyo mtu kafariki usiku hospitali. Kwahiyo ndugu zake wakishakuja ndo
watasema tunazikaje, kwa sababu alikuwa mkristo. Kwahiyo kwenye saa 7
mchana ratiba itakuwa tayari,” amesema Fela.
“Tatizo
alikuwa anaumwa kifua muda tu, lakini alishaanza kunywa dozi lakini
majuzi akazidiwa na tukampeleka hospitali. Jana ndo mwenyezi Mungu
kampenda zaidi akamchukua. Wazazi wa marehemu wapo Keko pale, lakini
wazazi wake baba na mama walifariki ila ndugu zake wapo, na kuna kibanda
waliachiwa na wazazi wake, kwahiyo msiba utakuwa Keko.”
Global Publishers tunatoa pole kwa familia ya Yesaya Ambilikile YP, ndugu jamaana marafiki, Bwana ametoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Post a Comment