Mwanariadha
wa Afrika Kusini Oscar Pistorius amehukumiwa jela miaka 5 baada ya
kupatikana na hatia ya kumuua mpenziwe Reeva Steenkamp.
Hii ni
baada ya mwanariadha huyo mlemavu kupatikana na hatia ya kumuua
mpenziwe Reeva Steenkamp mwaka uliopita bila ya kukusudia.
Jaji
aliyetoa hukumu hiyo,Thokozile Masipa,alianza kutoa kauli yake ya mwisho
kabla ya kutoa hukumu saa mbili na nusu asubuhi na akasema ni
changamoto kubwa kwake kupata adhabu ambayo itaridhisha pande zote
kwenye kesi hiyo.
Upande
wa mashitaka ulitaka mwanariadha huyo kupewa kifungo cha miaka 10
gerezani baada ya kupatikana na makosa ya kuua bila kukusudia.
Pistorius alisema kuwa alifyatua risasi baada ya kudhani kuwa jambazi alikuwa amevamia nyumba yake.
Upande
wa mashitaka unasisitiza afungwe jela wakati wakili wa Pistorius
wakimtaka jaji ampe kifgungo cha nyumbani cha miaka mitatu na pia apewe
usaidizi na ushauri wa kubadili tabia yake.
CHANZO:BBC
Post a Comment