Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule
(kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu wiki ya Umoja wa
Mataifa inayotarajiwa kuanza kuadhimishwa Ijumaa wiki hii (kushoto) ni
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
Na Mwandishi Wetu
KATIBU
MKUU wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, John Haule
amesema serikali ya Tanzania imefikia kwa kiwango kikubwa baadhi ya
malengo ya milenia ya afya na elimu. MOblog Tanzania inaripoti Akizungumza
katika mahojiano maalumu na MOblog Tanzania ofisini kwake jijini Dar es
Salaam baada ya kumaliza mkutano na wanahabari juu ya wiki ya Umoja wa
Mataifa inayotarajiwa kuanza Ijumaa wiki hii, Haule amesema Tanzania
imeyafikia kwa kiwango kikubwa malengo ya milenia katika afya na elimu.
“Serikali
ya awamu nne kwa kiwango kikubwa imefikia baadhi ya malengo ya milenia
hasa katika elimu na afya kwa kujenga shule za msingi na sekondari
katika kila kata na vituo vya afya nchi nzima,” amesema Haule.
Amesema
kwamba Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana kwa karibu na Umoja
wa Mataifa katika kufikia maendeleo katika kila nyanja duniani.
Aliongeza
kwamba ni muhimu nchi zote duniani kuendelea kushirikiana kwa pamoja
ili kuhakikisha maendeleo yanayopatikana yanapatikana kwa pamoja na
hakuna nchi inayoachwa nyuma.
Haule
alisisitiza kwamba katika kuadhimisha wiki ya Umoja wa Mataifa serikali
itaendelea kutoa ufafanuzi kwa wananchi umuhimu wa kushiriki kikamilifu
katika kila jambo linalofanya na Umoja wa Mataifa.
“Umoja
wa Mataifa unatimiza miaka 69 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1945
mafanikio mengi yamepatikana na changamoto bado zipo nyingi lakini nchi
zote wanachama wa Umoja wa Mataifa wataendelea kushirikiana na umoja huu
kutimiza lengo kuu la maendeleo dunia nzima,” alifafanua
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, John Haule akiteta jambo na Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
Amesema
kwamba katika mpango mkakati wa Umoja wa Mataifa juu ya malengo mapya
ya kuanzia mwaka 2015-2030 serikali imejipanga kuhakikisha malengo hayo
yanafikiwa kwa kiwango kikubwa.
Kwa
upande wake, Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na
mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini,
Alvaro Rodriguez, amesema kwamba Umoja wa Mataifa itaendelea
kushirikiana na nchi zote wanachama ikiwemo Tanzania katika harakati za
kuondoa umaskini.
“Malengo
ya milennia yamefanya nchi nyingi wanachama kufanya kazi kwa bidii
katika kupunguza umaskini wa kipato, fursa ya elimu na upatikanaji wa
matibabu kwa njia nafuu kwa maelfu ya watu duniani,”
Aliongeza
kwamba katika kauli mbiu ya Umoja wa Mataifa ya kuhakikisha kwamba
hakuna mtu anayeachwa nyuma katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii
inalenga kuwakutanisha pamoja nchi zote katika kila hatua ya maendeleo
dunia nzima.
Rodriguez
amesema kwamba Umoja wa Mataifa na malengo yake ni kuhakikisha usawa wa
kiuchumi na kijamii unafikiwa katika jamii pana iliyo huru kwa
kumshirikisha kila mtu katika maamuzi ya maendeleo.
Post a Comment