Mke
wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Watu wa China Ndugu Li Yuanchao wakati walipokutana kwenye Sherehe ya
kutimiza Miaka 50 ya Uhusiano wa Kidiplomasia baina ya Tanzania na
China. Sherehe hizo zilizoandaliwa na Ubalozi wa Tanzania nchini China
na kufanyika jijini Beijing.
Makamu
wa Rais wa China Ndugu Li Yuanchao akigonganisha glasi ikiwa ni ishara
ya kusherehekea kutimiza miaka 50 ya ushirikiano wa kidiplomasia kati
ya Tanzania na China. Sherehe hizo zilifanyika jijini Beijing.
Rais
Dkt. Jakaya Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa Ndugu Bernard Membe wakisherehekea kutimiza miaka 50 ya
Ushirikiano wa Kidiplomasia baina ya Tanzania na Cina kwa kugonganisha
glasi zao huku Mama Salma na Makamu wa Rais wa China Ndugu Li Yuanchao
(aliyesimama kulia) wakishuhudia. Sherehe hizo zilifanyika Beijing
nchini China tarehe 23.10.2014. PICHA NA JOHN LUKUWI
Post a Comment