Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu asiye na Wizara Mhe.Profesa Mark Mwandosya
akisalimiana na Makamu wa Rais wa Kenya Mhe William Ruto wakati wa
sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Zambia Mjini Lusaka jana.
Mhe. Mwandosya alimuwakilisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika sherehe
hizo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu
asiye na Wizara Mhe. Mark Mwandosya (wa tatu kulia ) pamoja na Mkewe
Lucy Mwandosya wakishiriki kuimba Wimbo wa Taifa wa Zambia wakati wa
sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Zambia Mjini Lusaka jana.
Wengine kutoka kulia ni Kaimu Rais wa Zambia Mhe Edgar Lungu ambaye pia
ni Waziri wa Ulinzi, na wa pili kulia ni Makamu wa Rais wa Nigeria
Monance Namadi Sambo.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu asiye na Wizara Mhe. Mark Mwandosya na
mkewe Lucy Mwandosya wakisalimiana na Rais wa kwanza wa Zambia Mzee
Kenneth Kaunda wakati wa sherehe za kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa
Zambia Mjini Lusaka jana. Mhe. Mwandosya alimuwakilisha Rais Jakaya
Mrisho Kikwete katika sherehe hizo ambazo zimefanyika Mjini Lusaka jana.
Picha na Mpiga Picha wete
Post a Comment