Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Soma Kwa Makini Kauli Rasmi ya Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Shy-Rose Bhanji Kuhusu Taarifa za Kutia Aibu


 Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Shy -Rose Bhanji
--
Chini ni Sehemu ya Taarifa ya Shutuma Juu yake
Tuhuma:

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EAC), Shyrose Bhanji kazua balaa kwenye kikao cha Bunge hilo mjini Kigali jana na leo! Walioandika trh 8 kwenda Brussels kwenye Bunge la EU members wote wa Tume yao na Wenyeviti wa Kamati. Wakiwa safarini kwenda ndani ya ndege sijuwi kukosa ile lishe aliyoizoea? Akawa anakunywa kama kichaa! Crews wakamzuia kuwa kwakuwa ndege ni ya mchana asinywe kupitiliza. Akaanza kutukana crews matusi yote unayoyajua!

Akawaambia hawajuwi kama yeye ni mbunge wa EAC? Akaanza kufanya fujo ndani ya ndege, akachukua chupa akapasua! Hapa security ndani ya ndege wakamkamata na kumtia pingu! Maneno yakawa yanamtoka ovyo. Wenzie walipojaribu kumtuliza wa kutoka Rwanda na mwingine Uganda (names withheld) akawageukia, tukana hadi marais wao hya kutosha! Hapo walikuwa juu ya anga ya Cairo.
Pilot akakataa kuendelea na safari akataka kushusha ndege Cairo. Walimsihi sana Pilot ndio akakubali kwa masharti Shyrose adhibitiwe!

Walipofika Brussels vituko havikuishia hapo. Kwenye mikutano anabwabwaja ovyo. Mbaya zaidi akaandika ki-note na kukiweka mgongoni ili walio row ya nyuma yake wakisome. Kiliandikwa kuhusu yule mbunge/Waziri wa EAC aliyefariki kuwa amekufa kwa UKIMWI, na kwa kuwa amelala na Wabunge wanawake wa EALA (kawaandika majina kwenye ki-note) nao wana UKIMWI kwa kuwa wanaumwa mara kwa mara.

Wakamaliza ziara ambayo hata Spika wa EALA alikuwepo, Wabunge toka Tz waliokuwepo pamoja na Shyrose ni Kimbisa na Angella Kizigha; kwa rekodi mbaya!

Sasa Bunge la EALA limeanza vikao juzi, jana Bunge limevunjika, hawataki kujadili Miswada wala nini hadi Shyrose ajadiliwe Bungeni kwa mambo ya aibu aliyoyafanya ktk ziara hiyo. Bunge likavunjika!

Leo asbh kulikuwa na kikao cha House Business, ambacho kwa huku Bongo ni kama Kamati ya uongozi. Agenda ni Shyrose na kuvunjika kwa Bunge jana. Kikao kimevunjika na Wajumbe wote wamejiuzulu! Wanasema kwanini Spika hakumkemea Shyrose alipofanya ujinga kwenye ndege? Kwanini hamuwajibishi kwa kumfukuza Bungeni ilhali anajua sifa zote mbaya za Shyrose tangu ameingia EALA? Sasa hivi wote wamejiuzulu na sasa si tu wanataka Shyrose afukuzwe bali na Spika ajiuzulu mara moja!

Wajumbe wanadai walipojitoa na kujiuzulu, Spika peke yake hajajitoa, hivyo naye aende na maji! Yaani hakuna kinachoendelea, Wabunge wanasema Bunge halitaendelea wala kufanyika hata kwa miaka 10 ijayo hadi Shyrose na Spika waondoke!

Hii ni aibu kubwa kwa nchi yetu! Kila Shyrose anapopita hukosi kusikia kapigana, kagombana, katukana au kufanya mambo ya aibu! Hapo EALA kagombana na watu wengi kuanzia Wabunge wenzie hadi staff.

Nitaendelea kuwajulisha kinachoendelea. Vilugho mnyetishie ta Nanka.

Fuatilieni website ya Eac na ile ya Bunge lao huwa wapo live www.eala.org
Majanga!

----------------
Chini ni Kauli Rasmi ya Mheshimiwa Shy-Rose Bhanji 

Kauli:

Mimi Shy-Rose Bhanji, Mbunge wa Afrika Mashariki-Tanzania, ninapinga vikali na kwa nguvu zote shutuma zilizotolewa dhidi yangu kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.

Shutuma hizi hazina ukweli wowote na zinalenga, si kuniharibia, bali kuchafua sifa yangu na utendaji kazi wangu katika Bunge la Afrika Mashariki.
Lengo kuu la shutuma hizo ni kunivunja nguvu na ari ya kutetea maslahi ya nchi yangu na Watanzania wenzangu kwani daima nimekuwa kikwazo na mwiba kwenye ajenda zinazokiuka maslahi ya Tanzania.

Kwa mfano ardhi ya Tanzania kugawiwa kwa wana Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kinyume na Sera ya Tanzania. Nimekuwa miongoni mwa wabunge wa Tanzania tulio mbele katika kulipinga suala hilo. Sishangai likinijengea uadui.

Isitoshe, kwenye ajenda ya kumuondoa madarakani Spika wa EALA, Dk. Margaret Zziwa, nilisimama kidete kwa kutounga mkono kwa sababu halikuwa na maslahi ya Tanzania na yalikuwa kinyume na malengo ya ushirikiano wa Jumuiya nzima.

Hoja ya kumuondoa Spika ilikuwa ni sehemu ya ‘mchezo mchafu’ ya ajenda ya siri ya kumweka kwenye nafasi hiyo mjumbe mwingine kwa maslahi ya wachache.

Jaribio hili la kumuondoka Spika lilifanywa na kushindikana mara tatu baada ya kukosa sahihi za kutosha kutoka Tanzania, ikiwamo ya kwangu.

Baada ya kampeni ya kumwondoa Spika kushindwa, wabunge kadhaa walikuwa wanasusia vikao vya Bunge wakati wameshachukua posho za vikao. Kwa mfano kikao kilichofanyika hivi karibuni hapa Dar es Salaam.

Malumbano ndio yamekuwa yakitawala na kuinyima Bunge akidi ya kuendelea na ajenda za mtangamano. Huu ni usaliti wa wazi kwa nchi zilizowachagua na kuwatuma katika Bunge la EALA.
Ukijaribu kuwaasa kwamba mwenendo huo si sahihi, unageuka kuwa adui.

Na sasa wameamua kunitukana na kuzusha tuhuma kadhaa kupitia mitandao ya kijamii ambako yote ni utunzi wa kisanii usiokuwa na chembe ya ukweli, uhalali wala ushahidi.

Wahenga walisema ‘akutukanaye hakuchagulii tusi’. Walete ushahidi wa tuhuma zote dhidi yangu.
Kwa mfano, shutuma kwamba nililewa pombe ndani ya ndege, kuvunja chupa, kufanya fujo na kufungwa pingu wakati wa safari ya Ubelgiji si kweli hata kidogo.

Kama hizi tuhuma ni za kweli, kwanini hazikupelekwa polisi, serikalini au vyombo vingine vya sheria baada tu ya tukio?

Ijewe wamesubiri wiki mbili baada ya madai hayo ya tukio la kutunga ndipo wajitokeze wakati wa kikao kinachoendelea mjini Kigali, Rwanda? Kwanini wasubiri kikao cha Kigali ndipo uzushi huu utolewe?

Tuhuma kwamba nimewatukana marais wa nchi tatu hazina mashiko isipokuwa kuhalalisha kampeni ya wale wanaonichafua na kuibua chuki kwa maraisi na raia katika nchi za Kenya, Rwanda na Burundi.

Ninayo heshima kubwa sana kwa marais wa nchi zote tano na raia wa nchi wanachama ambako mara zote nimepokewa na kuishi kwa amani na upendo katika nchi hizo. Naahidi kuedeleza heshima hii.

Hainiingii kichwani ni wapi nilipoteza heshima hii isipokuwa kwa wale wasionitakia mema ambao wamekusudia kufanikisha ajenda zao.

Shutuma zote dhidi yangu zimetengenezwa na watu ambao hatushabihiani katika hoja zetu na sishangai kwa hilo.

Mimi ni Mtanzania na ni Mbunge wa Tanzania. Hivyo nina wajibu wa kulinda na kutetea maslahi ya Watanzania ili kuleta mtangamano wenye uwiano sawa kwa nchi zote wanachama.

Ninaahidi nitaendelea kuwatumikia Watanzania kwa nguvu zangu zote na kutoa ushirikiano kwa wabunge wengine wa EALA kwa manufaa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Nimeyasema haya nikiamini kuwa: “Uongo ukiachwa usemwe mara nyingi unaweza kuaminiwa kuwa ni ukweli.”

Umoja Wetu Ni Nguzo Yetu
Mungu ibariki Afrika Mashariki
Asanteni,
Shy-Rose Bhanji
Mbunge EALA
 
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top