![](http://3.bp.blogspot.com/-_S5SVLGsTeo/VDYX7qdrdWI/AAAAAAAArZg/qeM6AIJ5m6A/s640/SADW.jpg)
Baba
mzazi wa marehemu Focus Saimon (9).Focus aliyekuwa akisoma darasa la
tatu katika Shule ya Msingi Kumbukumbu, amedaiwa kufanya tukio hilo
Jumamosi iliyopita kwa kufunga gauni la mdogo wake shingoni na
kujitundika kwenye komeo hilo mpaka kukata roho.
Katika
hali ya kushangaza, mtoto Focus Saimoni (9), mkazi wa Kwa Bibi Yuda,
Kinondoni jijini Dar amekutwa amejinyonga kwenye komeo la mlango wa
sebule yao.
Kwa mujibu wa chanzo makini, tukio hilo lilitokea saa 6 mchana wakati
wazazi wa mtoto huyo wakiwa kazini na kuacha ufunguo kwa mmiliki wa
nyumba aliyejulikana kwa jina la mama Fau.Chanzo hicho kilieleza kuwa
siku ya tukio, Focus alirejea nyumbani kutoka shuleni na kumuacha mdogo
wake, Irene Steve (5).
Akizungumzia tukio hilo, mtoto Irene alisema baada ya kumkuta Fucus akining’ing’inia hakuamini mara moja kama amefariki dunia.
Akizungumza na mwandishi wetu, mama mdogo wa Irene, Catherine Zakaria
alisema naye hakuamini tukio hilo.“Aliponiambia Focus kaning’inia
mlangoni nilishtuka, nikakakimbilia eneo la tukio na kukuta kweli.“Ila
mimi naamini kuna mtu alimnyonga kwa kutumia gauni la ndugu yake, nasema
wamemnyonga kwa sababu mazingira ya tukio asingeweza kujitundika juu ya
komeo mwenyewe kwa umri wake na kimo chake,’’ alisema Catherine.
Akizidi kufafanua juu ya mazingira aliyoyakuta, Catherine alisema
alishangaa wakati akihangaika kuita majirani, aliporudi aliukuta mwili
umeshushwa chini. “Niliukuta mwili wa marehemu ukiwa umening’inia juu ya
mlango lakini katika kutoka kuita majirani, kurudi nikakuta mwili
umeshushwa chini, nilipojaribu kuuliza ni nani aliyeushusha, hakuna
aliyenijibu,’’ alisema Catherine.Akizungumzia tukio hilo, mmiliki wa
nyumba hiyo, mama Fau, alisema alishtushwa na tukio hilo.
Mama wa marehemu, Rehema alisema anaumia kukuta mwanaye amefariki dunia na kuomba vyombo vya dola vifanye kazi yake kikamilifu.
Post a Comment