Mwanadada
asiyechuja kwenye muziki wa Bongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’
mwishoni mwa wiki iliyopita alibambwa ‘laivu’ kwa mara ya kwanza katika
kipindi kirefu akiwa ‘very close’ na mwanamuziki mwenzake, Ambwene
Yessaya ‘AY’ wakiteta jambo.Wabongo Fleva, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’
na Ambwene Yessaya ‘AY’ wakiteta jambo.
Ishu hiyo ilijiri kwenye Ukumbi wa High Spirit uliopo Jengo la IT
Plaza, Posta jijini Dar ambapo kulikuwa na uzinduzi wa huduma mpya ya
mtandao wa Airtelhuku mastaa mbalimbali na waandishi wa habari
wakijumuika pamoja kuanzia saa 1:00 usiku.
Mapema kabla ya uzinduzi huo, AY aliyekuwa amepiga pamba nyeusi
alikuwa wa kwanza kutinga ukumbini hapo akiwa ameongozana na Mtangazaji
wa Show ya Mkasi kupitia EATV, Salama Jabir.Wakiwa wanapiga stori za
hapa na pale, mara Jide naye alitinga ukumbini hapo ambapo jicho lake
lilitua kwa AY na kusogea karibu kwenda kusalimiana naye.
Wakiendelea kujadiliana.
Wakiwa katika maongezi Jide na AY, mshereheshaji aliyekuwa akiendesha
uzinduzi huo, Ephraim Kibonde aliwataka wakae mbele ikiwa ni kusaidia
kuendesha shughuli ya ufunguzi wa huduma hiyo kama majaji.
Katika uzinduzi huo, waandishi na wahudhuriaji walikuwa wakishindana
kuimba na kupewa zawadi kama head phones, simu aina ya Samsung Galaxy
III pamoja na spika ndogo kutoka kampuni kubwa ya kutengeneza bidhaa za
muziki iitwayo Beats.
Jide alionekana kukubali wito huo wa kukaa na AY ambapo aliamua
kuwatema wenzake aliokuwa ameongozana nao hapo ukumbini na kwenda kukaa
mbele na AY, vivyo hivyo kwa AY naye aliwatema akina Salama na mshikaji
wake na kwenda mbele.
Judith Wambura Mbibo ‘Jide’.
Katika hali nyingine ya kuduwaza, Jide akiwa na AY huku wakionekana
wako ‘dipu’ kwa mazungumzo kabla ya kuanza kuwajaji waimbaji, alionekana
kukolea na kinywaji alichokuwa anakunywa bila kutumia glasi (kupiga
tarumbeta) mwanzo mwisho.
Mara kwa mara wawili hao walikuwa bize wakiteta kwa sauti ya chini kwa takribani nusu saa.
Maneno yaliotumika kwenye picha ukurasa wa nyuma si halisi bali ni kama walikuwa wanasema.
Post a Comment