STAA
wa filamu Bongo, Wema Isaack Sepetu ameshindwa kujibu mapigo ya mwandani
wake Nasibu Abdul ‘Diamond’ kwa kutompa zawadi yoyote katika sherehe ya
siku yake ya kuzaliwa iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee
uliopo Posta jijini Dar.
Staa wa filamu Bongo, Wema Isaack Sepetu akiwa na mwandani wake Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Kutokana na msanii Diamond kumpa zawadi ya gari aina ya Nisani Morano
mwandani wake huyo katika siku yake ya kuzaliwa japo hakuwepo na
kumuachia mama yake amkabidhi, mashabiki wengi walikuwa na kiu ya kutaka
kujua ni kipi ambacho Wema angemzawadia mpenzi wake katika siku hiyo
ili kudhihirisha upendo wake ikiwemo kwa mashabiki kama alivyofanya
Diamond.Gari aina ya Nisani Morano iliyotolewa kama zawadi kwa Wema
kutoka kwa 'Diamond'.
Mpaka shughuli inaisha watu mbalimbali walijitokeza kutoa zawadi zao
hukuwengine wakimmwagia noti pamoja na menejimenti yake kumzawadia gari
aina yaBMW X6 lakini mwanadada huyo alishindwa kuonyesha makeke yake
mpaka mwisho wa shughuli na kubaki akijilaumu;
“Hee halafu sijui kwa nini mpaka shughuli imeisha eti sijatoka kumpa
zawadi baby wangu, sasa mbona hakuna aliyenikumbusha?” alisema Wema
mwisho wa shughuli hiyo.
Post a Comment