Mzee Manento enzi za uhai wake.
MSANII wa filamu za Kibongo, Mzee Manento amefariki dunia jana jioni akiwa jijini Dar es Salaam baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Mzee
Manento alikuwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo na mpaka mauti
yanamfika alikuwa amelazwa katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni
jijini Dar es Salaam.
Mzee
Manento atakumbukwa katika filamu alizocheza kama 'Hero of the Church',
'Dar to Lagos', 'Fake Pastor' na nyinginezo. Ndugu, jamaa na marafiki
kwa sasa wamekutana nyumbani kwa marehemu huko Kigogo, Dar kujadiliana
kuhusu taratibu za mazishi.
Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahali pema peponi. AMEEN!
Post a Comment