Rais
Jakaya Kikwete akimpa cheti cha uraia wa Tanzania, Loveness Ruhaga
(kulia) aliyekuwa Mkimbizi kutoka nchini Burundi katika hafla
iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Tabora leo.
Rais Kikwete alitoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi 162,156 na
kuwatangazia kuwa sasa wamekuwa raia halali wa Tanzania hivyo
wahakikishe wanafuata sheria zote za nchi na waepuke kufanya vurugu za
aina yoyote kwani wakikiuka
masharti hayo waweza kunyanganywa uraia huo. Wakimbizi hao walioingia nchini tangu mwaka 1972 walionyesha furaha kwa kuimba na kucheza vyimbo mbalimbali. Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.

Mwakilishi
Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce
Mends-Cole (kushoto) akimuonesha Rais Jakaya Kikwete (kulia) mchoro
unaoonesha jinsi wakimbizi wa Burundi walivyoingia nchini wakati
walipokuwa wanatoka nchini kwao mwaka 1972. Rais Kikwete alitoa vyeti
vya uraia kwa wakimbizi 162,156 waliokuwa raia wa Burundi katika hafla
iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkoa wa Tabora leo.
Katikati ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.
Rais
Jakaya Kikwete akizungumza baada ya kuwapa vyeti vya uraia wa Tanzania,
waliokuwa wakimbizi 162,156 kutoka nchini Burundi walioingia nchini
tangu mwaka 1972. Tukio la utoaji wa vyeti hivyo lilifanyika katika
ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora
mjini humo leo. Raia Kikwete katika hotuba yake aliwataka raia hao wapya kuwa waadilifu na kufuata sheria zote za nchi. Wanne kushoto ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe, wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil na kulia ni Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke.

Msoma
risala ambaye ni mwakilishi wa raia wapya 162,156 nchini ambao walikuwa
wakimbizi kutoka nchini Burundi, Dafroza Baragwimba akiisoma risala yao
mbele ya Rais Jakaya Kikwete (watatu kulia) wakati ya hafla ya utoaji
wa vyeti kwa raia hao. Rais Kikwete alitoa uraia kwa wakimbizi hao na
kuwataka wawe waadilifu na kufuata sheria zote za nchi. Wanne kulia ni
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe.
Rais
Jakaya Kikwete (wasita kushoto waliokaa), mabalozi na wawakilishi wa
mashirika ya kimataifa nchini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias
Chikawe (watano kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison
Mseke (watatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatma
Mwassa (wasita kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na sehemu ya raia wapya 162,156 wa Tanzania (nyuma waliosimama) baada ya kupewa vyeti vya uraia na Rais Kikwete katika hafla iliyofanyika katika ofisi
ya Mkuu wa Mkoa mjini humo. Picha zote na Felix Mwagara, wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Post a Comment