Afisa
Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania,Boniface Wambura
akizungumza na wanahabari,wakati akitangaza viingilio na utaratibu wa
kuingia uwanjani katika Mechi ya Watani wa Jadi,Simba na Yanga
unaotaraji kuchezwa Oktoba 18,2014 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.Picha na Othman Michuzi.
Kiingilio
cha chini kwenye mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na
Simba itakayochezwa Jumamosi (Oktoba 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam ni sh. 7,000.
Washabiki
watakaolipa kiingilio hicho ni wale watakaokaa viti vya rangi ya bluu
na kijani ambavyo jumla yake ni 36,693 katika uwanja huo wenye viti
57,558. Viingilio vingine ni sh. 10,000 kwa viti vya rangi ya chungwa,
sh. 20,000 kwa VIP B na C wakati VIP A itakuwa sh. 30,000.
Tiketi
zitakazotumika kwenye mechi hiyo ni za elektroniki, na zimeanza kuuzwa
jana (Oktoba 13 mwaka huu). Tiketi zinapatikana kwa mtandao wa M-PESA,
CRDB Simbanking na maduka ya CRDB Fahari Huduma ambayo yapo zaidi ya mia
moja sehemu mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Mechi
hiyo namba 27 itakayochezeshwa na mwamuzi Israel Mujuni Nkongo
akisaidiwa na John Kanyenye na Ferdinand Chacha itaanza saa 10 kamili
jioni. Kamishna wa mechi hiyo ni Salum Kikwamba kutoka mkoani
Kilimanjaro.
Washabiki
wanatakiwa kununua tiketi mapema, kwani hazitauzwa uwanjani siku ya
mechi. Milango yote ukiwemo ule wa upande wa Mbagala (Uwanja wa Ndani)
itafunguliwa kwa ajili ya washabiki, na itakuwa wazi kuanzia saa 4
asubuhi.
Magari
maalumu tu yenye stika ndiyo yatakayoruhusiwa kuingia uwanjani kwa
kupitia Barabara ya Mandela. Pia washabiki hawaruhusiwi kuingia uwanjani
wakiwa na silaha, vitu vya vyuma na mabegi makubwa. Barabara ya
kuingilia upande wa Chang’ombe itafungwa kwa watumiaji wa magari.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Post a Comment