Askari
wa jeshi la Wananchi la Tanzania (JWTZ) akimwadhibu kijana ambaye
hakuweza kufahamika jina lake mara moja, kwa kumpigisha mbizi kwenye
dimbwi la maji ya barabarani baada
ya kukutwa akiwa ametinga sare za Jeshi la Wananchi huku akipiga misele
mitaani wakati akitambua kuwa yeye si askari ni raia wa kawaida.
Kijana
huyo alikutana na adhabu hiyo kali kutoka kwa mjeda huyo baada ya
kumbaini kuwa si askari halisi ya jeshi la Tanzania wakati alipokamatwa
na kushindwa kutoa maelezo ya kuridhisha kuhusiana na swala zima la
kijeshi, na hapo ndipo alipoanza kuamuliwa kuvua mavazi hayo na kisha
kuaza kutumikia adhabu hiyo. Tukio hilo lilitokea hivi karibuni maeneo
ya Kariakoo jijini Dar es Salaam.
Kijana akiendelea kutumikia adhabu ya kupiga mbizi. Picha na Kamanda wa Matukio Blog.
Post a Comment