Mbunge
wa Jimbo la Peramiho Mh. Jenista Mhagama na wanavikundi vya uchumi wa
Kijiji cha Lugagala wakishangiria ujio wa Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar aliyefanya ziara ya kukagua miradi ya kiuchumi na maendeleo
katika kijiji pao.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiweka jiwe la msingi la
uanzishwaji wa majengo ya vikundi vya uchumi katika kijiji cha Muungano
Zomba Mkoani Ruvuma.
Balozi Seif akishiriki kazi za ujenzi wa Taifa katika Kituo cha Afya cha Kijiji cha Lugagala kata ya Kilagano Mkoani Ruvuma.
Mke
wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi
akiwapongeza wananchi wa Kijiji cha Lugagala kwenye Mkutano wa Hadhara
kwa ushiriki wao katika shughuli za kiuchumi.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Balozi Seif akiagana na Makamanda wa
vikosi mbali mbali vya ulinzi na usalama kwenye uwanja wa ndege wa
Songea mara baada ya kukamilisha ziara yake ya siku mbili Mkoani
Ruvuma. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.
****************************************************
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Serikali
itaendelea na juhudi zake katika kuona mazao ya wakulima vijijini hasa
chakula cha nafaka { Mahindi } yananunuliwa ili kuwaongezea uwezo
wa kimapato wakulima hao katika kyukabiliana na ukali wa maisha.
Balozi Seif
alisema hayo wakati akizungumza na Wananc hi wa Kijiji cha Lugagala
kwenye mkutano wa hadhara baada ya kushiriki kazi za ujenzi wa Kituo cha
Afya cha Kijiji hicho pamoja na kuweka jiwe la msingi la nyumba za
miradi ya vikundi vya uchumi katika Kijiji cha Muungano Zomba akiwa
katika ziara ya siku mbili Mkoani Ruvuma kukagua shughuli za kiuchumi,
ustawi wa jamii na maendeleo.
Alisema
Serikali haiwezi kuona nguvu za Wananchi zina potea bure bila ya kuunga
mkono hasa ikizingatia kwamba asilimia 90% ya Watanzania wote wanaishi
katika maeneo ya uzalishaji vijijini.
Alifahamisha
utafiti na uchunguzi wa kina utafanywa kupitia Halmashauri za Wilaya
zinazohusika na uzalishaji wa mazao hayo ya biashara ili kuwadhibiti
walanguzi wenye tabia ya kuwanyhonya wakulima kwa ujanja wa kununua
mazao yao kwa bei ya chini.
“
Serikali haitokubali kuwaachia walanguzi kuendesha mpango wa kuwanyonya
wakulima kwa kununua mazao yao kwa bei ya chini na wao wakaiuzia
Serikali kwa bei ya juu “. Alisema Balozi Seif.
Balozi
Seif alieleza kuwa tathmini itafanywa ili msimu ujao wa kilimo cha
nafaka wakulima watendewe na kukamilishiwa haki zao ili kupewa nguvu na
ari zaidi ya uzalishaji.
Akizungumza
na wana vikundi vya Kijiji cha Lugagala Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar aliwapongeza wananchi wa Kijiji cha Muungano Zomba kwa
kuanzisha vikundi vya kiuchumi vitakav yowakomboa kiuchumi hapo baadaye.
Balozi
Seif alisema uwamuzi wa wananchi hao kuanzisha vikundi hivyo umekuwa ni
jambo la busara wakielewa kwamba suala la ajira ambalo huwakumba zaidi
vijana limekuwa gumu hasa katika sekta za umma.
Aliwataka
wana vikundi hao lazima wawe makini katika mikutano yao ya tathmini kwa
kuondoa urasimu na wawe wazi jambao ambalo litaleta kuaminiana baina ya
wana vikundi hao.
Kuhusu
suala la Katiba Mpya iliyopendekezwa na Bunge Maalum la Katiba Balozi
Seif alisema viongozi pamoja wabune wenyewe waliousika na mchakato wa
kupati,kana kwa Katiba hiyo wataendeleza juhudi katika kuwapatia elimu
wananchi kujua faida ya kuipigia kura wakati utapowadia.
Alisisitiza
umuhimu wa kudumishwa kwa amani iliyopo Nchini kwa vile makundi yote
yaliyoshiriki mchakato huo yameonyesha kuridhika la Katiba hiyo
inayopendekezwa.
Balozi
Seif aliongeza kwamba wananchi wakati huu wanapaswa kujiepusha na
kasumba za upinzani ambazo malalamiko kwao imekuwa ni sehemu ya sera
inayopaswa kuachwa na wananchi hao.
Naye
Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi
alihimiza kwamba Kiongozi lazima awe mfano wa maendeleo ya jamii badala
ya kushabikia vurugu na siasa chafu.
Mama
Asha alisema siasa ni kwa Viongozi kusimamia juhudi na harakati za
kiuchumi na maendeleo za wale wanaowaongoza kwa lengo la kuwakomboa
kimaisha.
Akitoa
Taarifa fupi ya uanzishwaji wa vikundi hivyo vya kiuchumi Afisa
Mtendaji wa Kata ya Kilagano Bibi Pulkena Malekela alisema jumla ya
vikundi 71 vimeanzishwa katika kata hiyo ili akinamama viwasaidie katika
kujikwamua kiuchumi.
Bibi
Pulkena alisema kati ya vikundi hivyo 26 viko tayari kut oa huduma
vikipata msaada wa uwezeshaji kutoka Mbunge wa Jimbo la Peramiho Mh.
Jenista Mhagama.
Hata
hivyo Afisa Mtendaji huyo wa Kata ya Kilagano alielezea changamoto
zinazovikabili vikundi hivyo kwa hivi sasa akizitaja kuwa ni pamoja na
ukosefu wa mtaji pamoja na huduma za umeme.
Akitoa
msalamu zake mbunge wa Jimbo la Parameho ambae ndie mwenyeji wa ziara
hiyo Mh. Jenista Mhagama alisema Serikali ya Chama cha Mapinduzi
imefanya mengi katika kuwaletea maendeleo wananchi wake.
Mheshimiwa
Jenista Mhagama alieleza kwamba kero nyingi zilizokuwa zikiwakabili
wananchi katika sehemu mbali mbali hapa Nchini Mijini na Vijijini
zimepungua hasa huduma za maji safi, afya na elimu.
Katika
kuunga mkono juhudi za wananchi wa Mkoa wa Ruvuma Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alichangia Shilingi Milioni
1,500,000/- kusaidia Vikundi hivyo pamoja na kuahidi nguvu za uwezekaji
kwa majengo ya vikundi hivyo.
Balozi
Seif pia akachangia shilingi Milioni 1,500,000/- kuendeleza ujenzi wa
Kituo cha Afya cha Lugagala pamoja na kuahidi kutoa mifuko mia tano ya
saruji ya ujenzi wa kituo hicho.
Post a Comment