Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka jiwe la msingi kuzindua rasmi ujenzi wa barabara ya kilometa 16 kutoka Usagara hadi Kisesa mkoani Mwanza jana.Rais Kikwete yupo mkoani Mwanza kwa ziara ya kikazi ya siku tatu.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua daraja la Nyashishi lenye urefu wa mita 67 lililopo katika barabara ya Usagara Kisesa wakati alipokwenda kuweka jiwe la msingi ujenzi wa barabara kilometa 16 ya Kisesa hadi Usagara inayojengwa kwa kiwango cha lami jana.
Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli akimuongoza Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kukagua daraja la waenda kwa miguu huko Mabatini Mkoani Mwanza muda mfupi baada ya kulifungua.
Muonekano wa Daraja la waenda kwa miguu liliojengwa Mabatini huko Mwanza lililozinduliwa na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete. (picha na Freddy Maro)
Post a Comment