''Tulijua
kuna uwezekano wa kisa cha pili kuripotiwa ,na tumejitayarisha kwa
uwezekano huo''alisema Daktari David Lakey ambaye ni kamishna wa idara
ya afya katika jimbo la Texas.
Marehemu Dancun ambaye aliambukizwa ugonjwa huo nchini Liberia ,alifariki katika hospitali ya Dallas siku ya jumatano.
Hatahivyo jina la muhudumu huyo halikutajwa.
Bwana
Duncan alipatikana na virusi vya ugonjwa huo katika mji wa Dallas mnamo
tarehe 30 mwezi Septemba ,siku kumi baada ya kuwasili kutoka katika
ndege ya Monrovia kuelekea Brussels.
Lakini
licha ya kuwaeleza madaktari kwamba alisafiri kutoka nchini
Libya,aliagizwa kwenda nyumbani baada ya kupewa dawa za maumivu.
Lakini Duncan baadaye aliwekwa katika karantini katika hospitali hiyo ,na kufariki baadaye licha ya kupewa dawa za majaribio.
Haijulikani
iwapo afisa huyo aliyepatikana na virusi vya ugonjwa huo alikaribiana
na Duncan au la baada ya kuonyesha dalili ama wakati alipolazwa
hospitalini.
Afisa huyo alipatikana na homa siku ya ijumaa kabla ya kuwekwa katika karantini ili kufanyiwa ukaguzi.CHANZO BBC SWAHILI
Post a Comment