Stori: Deogratius Mongela
Mshtuko! Siku
chache baada ya kujiengua kwenye nafasi ya uenyekiti katika Klabu ya
Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ anadaiwa kufutwa
uanachama wa klabu hiyo.
Chanzo
cha ndani ya klabu hiyo kimepenyeza madai kuwa, wameamua kumvua
uanachama Steve kwani wanaona ni ‘kirusi’ ndani ya klabu kutokana na
mwenendo wake.
“Steve
amekuwa akiwashawishi baadhi ya memba wajiunge na upande wake, tofauti
na umoja wa Bongo Movie Unity, viongozi wameamua kumfuta kabisa
uanachama,” kilisema chanzo na kuongeza:
“Amewatangazia
wenzake vibaya juzikati alivyokwenda Dodoma kwenye sherehe za
kukabidhiwa kwa Rasimu ya Katiba Iliyopendekezwa kwa kuwaambia viongozi
wa serikali kwamba wasanii ambao hawakwenda mjini humo ni Ukawa wakati
si kweli.”
Baada
ya chanzo chetu kujiridhisha na data hizo za ndani, mwanahabari wetu
alimtafuta Steve Nyerere ili kujua anazungumziaje juu ya ishu hiyo ya
kuenguliwa klabuni na mtazamo kuhusu suala hilo, alipopatikana alikuwa
na haya ya kusema:
“Mimi
ni mwanachana wa Bongo Muvi kama nimefutwa sijui lakini ni mwanachama.
Kuhusu kuwasemea nilipokuwa Dodoma, ningewasemea mimi kama nani? Sina
cheo cha kuwasemea wenzangu.
Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na tafrani kubwa Bongo Muvi huku madai mengi yakielekezwa kwa Steve.CHANZO GPL
Post a Comment