Stori: Gladness Mallya
MSANII wa filamu Bongo, Wastara Juma amemuumbua msanii mwenzake Deogratius Shija baada ya kutoa taarifa zinazoonekana ni za uongo.
Awali
Wastara ambaye hivi karibuni alinyakua tuzo ya Muigizaji Bora wa Kike wa
mwaka kwenye tuzo za Action and Cuts, alimshukuru Mzee Majuto kwamba
ndiye aliyemtoa kisanaa jambo ambalo limemhuzunisha Shija na kusema
anashangaa kwa kuwa yeye ndiye aliyemtoa.
Kufuatia
maelezo hayo, Wastara amesema, taarifa aliyoitoa Shija ni ya uongo
kwani filamu ya kwanza kabisa alicheza na Mzee Majuto ndiyo maana
alimshukuru, ya pili alicheza na Frank Mwikongi na ya tatu ndiyo ya
Shija.
“Nimemshukuru
Mzee Majuto kwa kuwa ndiye wa kwanza kunitoa, huyo Shija nimecheza naye
filamu ya tatu, sasa anacholaumu nini? Mimi huwa sipendi lawama za
kijinga,” alisema Wastara.
Post a Comment