Staa wa muziki wa Nigeria, Panshak Zamani ‘Ice Prince’ kuoza akiwa na staa wa Kibongo, Jokate Mwegelo ‘Jojo’.
Kutoka moyoni!
‘Ubuyu’ mpya mjini ni madai ya staa wa muziki wa Nigeria, Panshak
Zamani ‘Ice Prince’ kuoza akilitamani penzi la staa wa Kibongo, Jokate
Mwegelo ‘Jojo’.
MNIGERIA ABEMBELEZAHabari kutoka kwa vyanzo makini zilidai kwamba, Mnigeria huyo amekuwa akiwasiliana na kumbembeleza Jokate usiku na mchana akiomba wawe pamoja kwa jinsi moyo unavyomtuma.
Ilidaiwa kwamba hivi karibuni, Ice Prince anayekimbiza na ngoma yake ya I Swear amekuwa akitumbukiza vipande vya video kwenye ukurasa wake wa kijamii wa Instagram akimsifia Jokate ambaye anapendelea zaidi kumwita Kidoti.
ICE PRINCE: I MISS YOU KIDOTI!
Ilisemekana kwamba katika moja ya video hizo jamaa huyo anayefanya kazi na Jokate kwenye Runinga ya Chanel O nchini Afrika Kusuni ‘Sauz’ alisikika akimwambia mwadada huyo; ‘I miss you Kidoti’.
CHANZO CHATIRIRIKA
“Jamaa amemzimika Jokate ile mbaya. Unaambia anapiga simu na kumwita Jokate Sauz kila siku.
“Jamaa kafa kaoza. Kama unasikia mahaba niue ndiyo hayo sasa. Ishu ipo kwa Jokate tu kumkubali maana Ice Prince amekuwa akimuahidi kumpa maisha ayatakayo mtoto wa kike. Kazi anayo bidada, aamue kusuka au kunyoa,” alisema mmoja wa watu wa karibu wa Jokate.
JOKATE ABANWA
Baada ya kunyetishiwa ‘mchele huo ulionyooka’ Ijumaa Wikienda, gazeti namba moja la mastaa Bongo lilimsaka Jokate ambapo aliulizwa juu ya uhusiano wake na mwanamuziki Ice Prince na iwapo anajua kuwa ana mapenzi na yeye na kama akimtamkia ndoa, je, atakubali?
Huku akionekana kushtushwa na habari hiyo, Jokate alisema kwamba iwapo Ice Prince atamwambia jambo hilo, atamchunguza tabia zake na kama zitamridhisha basi hana shaka atamkubalia.
MWANAMKE SHURTI APENDWE
Jokate alisema kwamba mwanamke kupendwa ni habari nzuri, ingawa hadi sasa bado hajaona wa kumuoa.
BOFYA HAPA KUMSIKIA KIDOTI
“Sijaona bado wa kunioa lakini kama Ice Prince ana nia, nitamchunguza kama anafaa ishallah,” alisema Jokate huku akicheka.
ATAKA MTOTO
Kwa upande mwingine staa huyo wa sinema na Bongo Fleva alisema kwa sasa matamanio yake yote anahitaji mtoto kutokana na umri wake (miaka 27) kuzidi kuyoyoma.
Kwa upande mwingine staa huyo wa sinema na Bongo Fleva alisema kwa sasa matamanio yake yote anahitaji mtoto kutokana na umri wake (miaka 27) kuzidi kuyoyoma.
BABA BORA MPO?
Jokate alisema kuwa kama kweli akijitokeza baba bora (husband material) atazaa haraka.
Mwanadashoti alisema kwamba, yeye kama msichana, anatamani siku moja aitwe mama na kila akikaa anapata mawazo ya kuzaa lakini anashindwa kwa sababu Mungu bado hajamjalia mume ambaye atazaa naye.
“Natamani mtoto kiukweli basi tu ni Mungu anapanga ndoa lakini akinijalia tu mimi nitazaa mapema, sitasubiri ndoa yangu ikae sana kama wanavyofanya wanandoa wengine,” alisema Jokate.
KUKUTANA CHANEL O
Jokate mwenye mipango lukuki na bidhaa za Kidoti na Ice Prince wanatarajia kukutana kwenye kipindi kipya cha Runinga ya Channel O kinachokwenda kwa jina la Top Ten Most na huko ndiko kitaeleweka.
KWENYE ‘PROFAILI’ YA JOKATE
Huko nyuma Jojo aliwahi kuhusishwa kutoka kimapenzi na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Mbongo ambaye ni staa wa Mpira wa Kikapu (NBA) nchini Marekani, Hasheem Thabeet Manka.
Post a Comment