Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’ akwa ameshika gauni la mpenzi wake.
Imebumburuka kwamba staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul Juma ‘Diamond’
kumbe anateseka na penzi la mwandani wake, Beautiful Onyinye Wema Isaac
Sepetu, Amani lina mkanda kamili.
Kwa muda mrefu kumekuwa na madai kuwa, Diamond amekuwa akiumia na
kuvumilia anapoitwa majina mabaya huku akisemekana hamuwezi Wema hivyo
awaachie mapedeshee wenye ‘kisu’ kirefu.
“Hivi unajua kwa nini Diamond alimpa Wema zawadi ya Nissan Murano
(gari)? Alijua asipofanya hivyo kuna mtu atafanya na kweli ndivyo
ilivyotokea kwa lile Gari BMW.“Nawahakikishieni kwa Chibu au Dangote
(Diamond) alichezwa na machale,” kilidai chanzo chetu ambacho ni mtu wa
karibu wa wawili hao.
Sasa ndani ya pati ya bethidei ya Diamond kwenye Ukumbi wa Golden
Jubilee uliopo Posta jijini Dar mwishoni mwa wiki iliyopita, kidume huyo
alinaswa akiwa ameshikilia gauni la Wema kwa muda mrefu ili kuhakikisha
haliburuzi chini kwa urefu.
Akimshikia gauni la mpenzi wake huku wakiingia ukumbini
Wakati wa kukabidhiwa zawadi ya gari aina ya BMW X6 alilopewa na
menejimenti yake, ndipo kulipokuwa na sarakasi kubwa kati ya mastaa
hao.
Baada ya wageni waalikwa kutangaziwa kuwa kuna zawadi maalum ya jamaa
huyo, watu waliombwa kutoka nje kuelekea eneo la maegesho ya magari
(parking) ili kushuhudia makabidhiano hayo.
Hapo ndipo Diamond alipojikuta akihangaika zaidi na gauni refu la
Wema akilishikilia na mkono mmoja huku mwingine ukiwa umeshika glasi ya
‘waini’ nyekundu.
Wakati wakitembea mdogomdogo kama maharusi, Diamond alijikuta akiwa
kama mpambe wa bibi harusi kwa kumzunguka Wema mara kwa mara
akilishikilia gauni hilo, shukurani ziende kwa mbunifu wake maana mtoto
wa kike alitokelezea mashalaah!
Diamond akimuweka sawa mpenzi wake.
UPAJA WA WEMA NJE
Kuna wakati Diamond alilinyanyua gauni hilo na kusababisha ule upaja
mweupe wa Wema kuwa nje huku midume ikiutolea udenda na wengine wakihisi
jamaa huyo alifanya makusudi ‘kuwaringishia’.
“Ebwana Chibu mbona anamfunua Madam upaja unaonekana? Au
anaturingishia ili tujue anakaa pazuri?” alisikika mmoja wa wanaume hao
bila kufafanua kukaa pazuri alimaanisha nini.
WEMA ACHEKELEA, ATEMBEA POLEPOLE
Wakati Diamond akihangaika na gauni hilo, Wema alikuwa akichekelea
kwa kuonesha uso wa tabasamu na kutembea polepole ili kumhenyesha staa
huyo na kuthibisha kwamba kweli yeye ni Madam na kwamba Diamond anajua
‘kukea’.
Wema na Diamond wakifanya yao.
KIJASHO CHEMBAMBA CHAMTOKA DIAMOND
Hadi wanafika kwenye zawadi hiyo ya gari, kijasho chembamba kilimtoka
Diamond ambaye alipokea ufunguo kwa mkono mmoja baada ya kuomba
ashikiwe glasi ya ‘waini’ huku mkono mwingine ukiendelea kushikilia
gauni hilo hadi alipomfungulia Wema mlango akaingia, naye akazunguka
upande wa dereva.
Baada ya kulitesti gari hilo lenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni
90, wawili hao walirejea ukumbini kwa staili ileile ya Diamond
kuhangaishwa na gauni hilo hadi walipoketi meza kuu na kuendelea na
ratiba.
NI ‘KAMZIZI’?
Kwa mujibu wa watu wapenda ‘ubuyu’ waliokuwemo ukumbini humo
walisikika wakisema si bure, Diamond kuhangaika na Wema kiasi hicho
hivyo huenda kawekewa ‘kamzizi’.
“Mimi nakwambia hata kama ni kumpenda kiasi gani lakini hii ni zaidi
ya mahaba niue au kawekewa kamzizi, si bure kwa wanaume wa kizazi hiki
kukea kiasi hiki,” alisikika mmoja wa wanawake waliokuwa wakimuonea wivu
Wema na kumpa pole Diamond kwa kuhenya.
Post a Comment