Kioo cha lori cha mbele kikiwa kimepasuka.
WATU watatu
akiwemo dereva wa gari la kampuni ya soda ya Coca Cola walipata
michubuko kadhaa katika ajali iliyotokea leo asubuhi maeneo ya Lugalo,
jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na mtandao huu, mmoja wa mashuhuda amesema chanzo cha ajali hiyo ni
baada ya gari ndogo kuingia ghafla mbele ya gari hilo kubwa lililokuwa
limebeba vinywaji na ndipo gari kubwa likiwa katika kukwepa likajikuta
likianguka ubavu.
(Habari/Picha na: Gabriel Ng’osha/GPL)
Post a Comment