Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

TAARIFA YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU

a4
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatarajia kupokea mwili wa Marehemu Meja Jenerali Muhidini Mfaume Kimario (Mstaafu) kutoka nchini India leo tarehe 09 Oktoba, 2014 katika uwanja wa Kimataifa wa Mwl JK Nyerere Dar es salaam mwili wa marehemu utawasili kwa Shirika la ndege la Ethiopia saa 7:30 mchana.
Mwili wa marehemu utaagwa kesho tarehe 10 Oktoba, 2014 saa 4:00 asubuhi katika viwanja vya hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo na baadaye mwili utasafirishwa kwenda kwao Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro kwa mazishi yatakayofanyika tarehe 11 Oktoba, 2014 saa 7:00 mchana siku ya Jumamosi.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mh. Dkt Hussein Mwinyi anatarajiwa kuongoza waombolezaji kutoa heshima za mwisho.
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU
MEJA JENERALI MUHIDINI KIMARIO (MSTAAFU)
AMINA
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top