Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Mkurugenzi Mtenda wa Shirika la
Maendeleo ya Petroli la Oman (PDO), Bw. Raoul Resticci baada ya kuwasili
kwenye makao makuu ya Shirika hilo ili kujifunza shughuli za uwekezaji
na uvunaji wa gesi na mafuta . Alikuwa katika ziara ya kikazi nchi
OmanOktoba 28, 2014.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na baadhi ya mabalozi wanaowakilisha
wa nchi mbalimbali nchini Oman katika dhifa aliyoandaliwa na Naibu
Waziri Mkuu wa Oman, Mhe. Sayyid Fahad Al Said (kulia) kwenye hoteli ya
Al Bustan mjini Muscut Oktoba 29, 2014.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda na Naibu Waziri Mkuu wa Oman, Mhe. Sayyi Fahad Al
Said (kushoto kwake) wakizungumza na balozi wa Tanzania nchini Oman,
Ali Ahmed Saleh katika dhifa aliyoandaliwa Waziri Mkuu kwenye hoteli ya
Al Bustan mjini Muscut Oktoba 28, 2014. Wapili kulia ni Waziri wa Mifugo
na Uvuvi, Dr. Titus kamani na watatu kulia ni Naibu Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Maalim Mahadhi.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiweka saini kitabu cha wageni baada ya kutembelea
msikiti wa Sultan Qamboos Grand uliopo Muscut ambao ni kati ya misikiti
mikubwa na inayovutia duniani Octoba 29, 2014. Kushoto ni Mkurugenzi wa
Habari na Uhusiano wa serikali ya Oman, Ahmed Bin Salim Al Harthy.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akipokea kutoka kwa Mkurugenzi wa Habari na
Uhusiano wa serikali ya Oman, Ahmed Bin Salim Ali Harthy zawadi ya
kitabu kinachoonyesha Msikiti wa Sultan Qamboos Grand uliopo Muscut
baada ya kuutembelea msikiti huo akiwa katika ziara ya kikazi nchini
Oman, Oktoba 29, 2014
Mke
wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda akipokea kutoka kwa Mkurugenzi wa
Idara ya Habari na Uhusiano wa Serikali ya Oman, Ahmed Bin Salim Al
Harthy zawadi ya kitabu baada ya kutembelea msikiti wa Sultan Qamboos
Grand wa Muscut ambao ni kati ya misikiti mikubwa na yenye kuvutia
duniani.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
akizungumza na mmoja wa wafanyabiara wa Oman wanaokusudia kuwekeza
Tanzania, Sheikh Abdullah Al- Zakwani baada ya kikao chake na
wafanyabiashara wa Oman kwenye hoteli ya Al Bustan, Muscut Oktoba 29,
2014.
Waziri Mkuu, MIzengo Pinda
akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Uhusiano wa Serikali ya
Oman , Ahmed Bin Salim Al Harthy baada ya kutembelea Msikiti wa Sultan
Qaboos Grand uliopo Muscut ambao ni moja kati ya misiki mikubwa na yenye
kuvutia sana dunianiOktoba 29, 2014. Kulia ni balozi wa Tanzania nchini
Oman, Ali Ahmed Saleh.Yuko katika ziara ya kikazi nchini Oman
Post a Comment