![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg4Sk1Za3TKMutxiP3P81GIrgbqVl5lR2EilnxXUCAjjFR6Ko24GLLrGc-o_jMTA8vkg1ot4hBXiTwxbnLEiTfZY4uWV6blM5bi1fqXFYxrf0ZfYtNN91fzrYSpaUZ1VjUwCOOj6gzTiIwb/s1600/10818625_10154825415810247_1542609338_n.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjTs-P6dXymeD0T1kvQK3aOx4cNHISO23YIvhhkxSMaHA2vUUkmLG3ZH5zeQwqaxL8ryye9KXzpoytjpv3L8ydpuKl8QzHge6d-bGKirvKqgyCZBk4EeqrtfjmRzC-PwFGDbOd8dkm1za4P/s1600/10815677_10154825415795247_2063630105_n.jpg)
Pichani kijana Suleiman Othuman akiwa amelazwa hospitali ya Mnazi Mmoja wodi ya chini upande wa dirisha la dawa kitanda no 12.
Assalam
Aleikum ndugu zangu mnaotusoma kwenye blog hii kila siku, msaada
unahitajika kwa kijana Suleiman Othman Ally mwenye umri wa miaka 19,
mkaazi wa Zanzibar, amepatwa na tatizo la uvimbe mkubwa kwenye mgongo
wake baada ya kupatwa na ajali kugongwa na Vespa kwa muda wa siku
nyingi tu, walimpeleka Hospitali ya Mnazi mmoja ambapo ilishindikana
kupata matibabu kutokana na damu nyingi aliotoka wakati wa upasuaji,
hivyo kuwalazimu kumshona bila ya kumfanyia operation iliyokuwa
wamemkusudia.
Kijana
Suleiman Othuman hali yake inazidi kudhoofika na maumivu makali
alionayo kwa sasa hawezi kukaa kusimama vizuri na hata kulala
inavyostahiki kwa sababu ya ule uvimbe aliokuwa nao kwenye kiuno chake
kam picha inavyojionyesha.
Hivi
sasa familia yake haina budi kuomba ushirikiano wa msaada wenu kwa ajili
ya kumgharamia mtu mmoja wa familia kufuatana nae nchini India
kwaajili ya matibabu, kutokana na gharama ni kubwa na uwezo ni mdogo.
Hivi sasa yuko hospitali ya Mnazi Mmoja wodi ya chini upande wa dirisha la dawa kitanda no 12.
Ndugu zangu tujitahidini kuokoa maisha ya ndugu yetu Suleiman Othuman kwa hali na mali. Kwa
mtu yoyote atakayeguswa na habari hii, na mwenye kutaka kuchangia
msaada wake anaweza kuwasiliana na Mama yake mkubwa. Bi Salma.
Numba yaze za simu ni-:
255777489015
Tigo: 255655489015
Pia unaweza kuwasiliana na Mdau wa Blog Hii Abou Shatry Number 301-278, 3977,
Email swahilivilla@gmail.com
Post a Comment