Katibu
wa Uhamasishaji Umoja wa Vijana wa CCM, Paul Makonda akionesha kwenye
simu yake picha ya video iliyopigwa wakati wa vurugu zilizotokea wakati
wa mdahalo wa kujadili raismu ya Katiba inayopendekezwa, kwenye Ukumbi
wa Ubungo Plaza jana, ambapo Makonda aliyedaiwa kumpiga aliyekuwa
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Waziri Mkuu wa zamani Jaji
mstaafu Joseph Warioba, amekanusha kumpiga leo katika mkutano wa
waandishi wa habari, Dar es Salaam. Pia Makonda amesema kuwa hawezi
kabisa kudiriki kumpiga kwani anamheshimu kama babake mzazi. Amesema
kuwa hata leo asubuhi amezungumza na warioba kwenye simu kumjulia hali.
Warioba naye amekanusha kupigwa na Makonda wala mtu yoyote kwenye vurugu
hizo.
Makonda akisisitiza jambo katika mkutano huo ambapo pia aliwaambia kazi
kubwa aliyoifanya wakati wa vurugu hizo, ni kumsaidia Warioba kutoka
salama pamoja na Mwanasiasa mwenye ulemavu wa macho ambaye pia alikuwa
anamuokoa ili asipatwe na dhahama hiyo.
Makonda
akiendelea kuelezea kuwa anasikitishwa na vyombo vya habari ikiwemo
mitandao ya kijamii iliyomzulia kwamba yeye ndieye aliyesababisha vurugu
wakati siyo. Pia amelaani watu wote waliosababisha vurugu hizo kwamba
kitendo hizho kinadhoofisha demokrasia nchini. Habari, picha na Richard
Mwaikenda wa Kamanda wa Matukio blog
on Tuesday, November 4, 2014
Post a Comment