ACHANA na
mazingira ya kifo cha Bilionea maarufu wa Bukoba, Leonard Mtensa
aliyefariki saa chache baada ya kufanya mapenzi ndani ya gari kuacha
gumzo, gumzo lingine lilitokea wakati wa mazishi yake ambayo
yalihudhuriwa na wananchi wengi kutoka ndani na nje ya mkoa, mkanda
kamili huu hapa.
Kwa
mujibu wa chanzo kilichoshuhudia mazishi hayo mwanzo mwisho, msiba huo
ulikuwa wa pekee kwani haijawahi kutokea kwa yeyote kuzikwa na umati
mkubwa kiasi hicho na kusababisha watu wote wasimame kiasi cha kuwafanya
askari wa usalama barabarani kufanya kazi ya ziada kuhakikisha mambo
yanakwenda sawa.
“Ilikuwa
si mchezo, hii ni historia kwa Bukoba. Haijawahi kutokea msiba wa mtu wa
kawaida ukawasababisha watu kujipanga barabarani, trafiki kuongoza
harakati utafikiri mapokezi ya rais,” kilisema chanzo.
Inadaiwa
kuwa msafara wa magari ulivunja rekodi kwani wakati magari mengine
yalikuwa yameshafika makaburini, mengine yalikuwa bado kwenye foleni
nyumbani.
Jeneza likibebwa kuelekea makabulini.
Chanzo hicho kilizidi kupasha habari kuwa, msafara wa kutoka nyumbani kwa marehemu, Bukoba mjini hadi katika Kijiji cha Kyaikalabwa ambacho kipo umbali wa kilomita 3, ulikuwa mrefu kiasi ambacho magari yalijipanga kuanzia mjini hadi kaburini.
Post a Comment