Denis Mtima na Gabriel Ng’osha
LILE
sakata la mtoto wa miezi 6 (pichani) kufia mahabusu ya Kituo cha Polisi
cha Kova, Mbezi Kwamsuguri, Dar linaendelea! Safari hii, mama wa mtoto
huyo, Meradi Meshack ameibua mazito akiwataja polisi jamii kuwa ndiyo
chanzo cha kifo cha mwanaye.
Mtoto Thomas wa miezi 6 aliyefia mahabusu ya Kituo cha Polisi cha Kova, Mbezi Kwamsuguri, Dar enzi za uhai wake.
Awali
ilibainika kuwa, mtoto huyo aliyefariki dunia Novemba 18, mwaka huu
wakati mama yake akiwa amewekwa kituoni hapo kama mhalifu, polisi wa
kituo hicho walitajwa kuhusika.
Akizungumza
na waandishi wetu, mama huyo alisema yeye na mtuhumiwa wake aliyemtaja
kwa jina la mama Na walikuwa wakidaiana fedha za upatu ambazo alikuwa
akimdanganya kuwa wanachama wenzake bado hawajatoa.
Mama wa mtoto huyo akilia kwa uchungu msibani.
Baada ya usumbufu wa muda mrefu ndipo wakapishana maneno, mwanamke huyo akampeleka polisi akidai alitaka kumpiga
Post a Comment