Matukio ya
mimba za utotoni yamekuwa yakijitokeza kila kukicha yakiwa na sura
tofauti, mengi yametajwa kuharibu maisha na kupoteza ndoto za wasichana
wengi.
Kutoka
Nigeria Mzee mwenye umri wa miaka 75 anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa
kosa la kumpa ujauzito mwanafunzi mwenye umri wa miaka 13.Mzee huyo Pa
Alabi ambaye ni fundi seremala aliombwa na binti huyo kumtengenezea
kiboksi cha kuhifadhia pesa zake, baada ya kumpa kiboksi hicho akaanza
kumtongoza na kujenga ukaribu nae hadi binti akakubali.
“..Siku
yenyewe nilimwelezea hisia zangu na akaahidi kulifikiria suala hilo na
baadae akakubali, tulikutana kimwili pale nilipomuomba na tulikuwa
tukiheshimiana, ghafla akaacha kuja kwangu baada ya siku tano baada ya
ile siku ya kwanza tulipokutana kimwili. Siku moja akaja na kuniambia
Bibi yake alimwambia ni mjamzito ndipo alipoacha kuja kwangu na
sikumuona tena hadi Polisi walipokuja kunikamata.
Post a Comment