
Kituo cha michezo
kinajengwa kwa ufadhili wa Klabu ya Sunderland kwa kushirikiana na Symbion
Power na Serikali ya Tanzania.
Shehere hizo
zinatarajiwa kesho asubuhi (Jumamosi tarehe 1 Novemba 2014) kuanzia majira ya
saa mbili asubuhi.
Kwa mujibu wa taarifa
iliyotolewa leo jijini Dar es salaam na Mwakilishi wa Symbion nchini Julie
Foster , sherehe hizo pia zitahudhuriwa na Waziri wa Habari , Vijana ,
Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella E. Mukangara,
Afisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Sunderland ya Nchini Uingereza Bi. Margaret Byrne
na Afisa Mtendaji Mkuu wa Symbion Power
Bw. Paul Hinks
Taarifa hiyo imeongeza
kuwa pamoja na uzinduzi wa ujenzi huo Rais Kikwete atapanda mti kwenye eneo
hilo, akisaidiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Sunderland AFC Bi. Byrne, Mkurugenzi
wa Biasharawa klabu hiyo Gary Hutchinson, na Afisa Mtendaji Mkuu wa Symbion
Power Bw. Hinks,.
Klabu ya Ligi Kuu ya
Uingereza ya Barclays, Sunderland AFC inatoa usaidizi wa kiufundi na utendaji
katika uendelezaji wa mradi wa mpira wa miguu, ambao ni wa kwanza na wa aina
yake nchini humu, utakaohakikisha maelfu
ya vijana wananufaika kutokana na mtazamo wa pamoja wa kuchanganya mpira wa
miguu, elimu na ushiriki wa jamii, ili kupata ujuzi na utaalam wa Sunderland
AFC.
Post a Comment