
Mkurugenzi wa Ajira toka Wizara ya kazi na Ajira Bw.Ally Msaki
akiongea na waandishi wa habari kuhusu kasi ya uzalishaji wa nafasi za
ajira nchini ambapo katika kipindi cha miezi 3 kuanzia Julai hadi
Septemba 2014 jumla ya ajira 139,361 zimezalishwa. Kushoto ni Msemaji wa
Wizara hiyo Ridhiwani Wema

Msemaji wa Wizara ya Kazi na Ajira Bw. Ridhiwani Wema akiwaeleza
waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mikakati ya Serikali
kuendelea kuweka mazingira wezeshi ya waajiri kuongeza fursa za ajira
hapa nchini.kushoto ni Afisa Kazi Mkuu Bi Amina Likungwala.Picha na Frank Mvungi
-----
Na Frank Mvungi
Na Frank Mvungi
Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuimarisha mazingira ya
uzalishaji ajira katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita ambapo ajira
139,361 zimezalishwa.
Hayo yamesemwa na
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Wizara ya kazi na Ajira Bw.
Ridhiwani Wema wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar
es salaam.
Akizungumza
katika Mkutano huo Wema alisema kuwa kati ya ajira zilizozalishwa 3,657
ni ajira za Serikalini na 135,704 ni ajira kupitia sekta binafsi.
Akifafanua zaidi
Wema amesema, kwa kipindi cha mwaka 2011/12 ajira zilizolalishwa ni
250,678 ambapo mwaka 2012/2013 zilizalishwa ajira 274,030.
Kwa mwaka
2013/2014 ajira 408,756 zilizalishwa na mwaka 2014/15 jumla ya ajira
560,000 zilitarajiwa kuzalishwa katika sekta binafsi rasmi.
Aidha katika kipindi cha mwaka 2013/14 sekta
binafsi rasmi imezalisha ajira 408,706 kupitia uwekezaji binafsi ambapo
baadhi ya maeneo hayo ni Viwanda vidogo na kati ,Uwekezaji kupitia
TIC,Sekta ya Mawasiliano na nyingine.
Takwimu hizi zinaonyesha kuwa sekta binafsi
itafanya vizuri zaidi kwa kuwa Serikali imeendelea kuweka mazingira
wezeshi kwa waajiri ili waweze kuongeza fursa za ajira hapa nchini
ambapo baadhi ya hatua zinazochukuliwa kwa sasa ni pamoja na kufanya
marekebisho ya Sera ya Ajira ya mwaka 2008,Sheria ya Ajira na Mahusiano
Kazini No. 6 ya mwaka 2004.
Marekebisho
mengine yanayofanyika
yanahusisha sheria ya Taasisi za Kazi na Ajira Na.7 ya mwaka 2004 pamoja
na kutunga sheria mpya ya ajira za wageni Nchini ambayo imelenga
kulinga ajira za watanzania,kuboresha mazingira ya Biashara na
kuhamasisha uwekezaji.
Post a Comment