PICHA KUTOKA MAKTABA
Na Shija Felician
Kijukuu Blog Kahama
Maisha ya
wananchi wa kata ya mwendakulima wanaozunguka mgodi wa Buzwagi wilayani
Kahama mkoani Shinyanga yako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko
kutokana na kunywa maji yenye mchanganyiko na kinyesi cha binadamu
Hali
hiyo imebainishwa leo kwenye mkutano wa hadhara wa kamati ya bunge
Ardhi maliasili na mazingira ambao wananchi hao walihoji uhalali wa
walinzi wa mgodi wa Buzwagi kumwaga maji safi yanayochotwa kwenye eneo
linalomilikiwa na mgodi huo
Katika
mkutano huo wananchi hao wamedai maeneo ya visima vya kuchota maji
yamebanwa na matumizi ya kibinadamu hali ambayo baadhi ya vinyesi vya
binadamu hutiririka na kujichanganya kwenye maji hayo hali ambayo ni
hatari kwa maisha ya binadamu
Walisema
kutokana na hali hiyo visima vyenye maji safi na salama viko kwenye
eneo linalomilikiwa na mgodi wa Buzwagi lakini wananchi wakienda kuchota
humo maji hayo humwagwa na walinzi wa mgodi huo
Hata hivyo
malalamiko hayo mwenyekiti wa kamati hiyo James Lembeli amemtaka naibu
waziri wa bunge Ardhi maliasili na mazingira Ummy Mwalimu kulitolea
ufafanuzi lalamiko hilo kwa kuwa suala la uchafuzi wa maji liko kwenye
wizara yake
Kwa
upande wake naibu waziri huyo aliyekuwa ameambatana na kamati hiyo
kuzungukia migodi ya dhahabu amesema suala la ujenzi wa visima vya maji
salama sio la mgodi bali ni la halimashauri yao ya mji ni suala la
serikali ya kijiji kupeleka mipango kazi ya kujengewa visima
Post a Comment