Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

VAN GAAL AMPA ZA USO SMALLING, AMKINGIA KIFUA FELLAINI!

Manchester United imejikuta ikiindelea kuwa wanyonge wa Manchester City baada ya kukubali kipigo cha 1-0 katika mchezo mkali uliofanyika katika uwanja wa Etihad, Jumapili, goli lililofungwa na Sergio Aguero dakika ya 63. 

Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal amemlaumu beki wake Chris Smalling kwa kitendo cha kutolewa akidai kilikuwa cha ‘kijinga’. 
Smalling alitolewa kabla ya mapumziko kwa kupewa kadi mbili ya kwanza kwa kuzuia mpira wa mlinda mlango wa Man City, Joe Hart, ya pili ni kwa kumkaba vibaya James Milner. “Kwenye mechi kama ya dabi lazima uwe makini kadi ya pili ya njano ilikuwa ya kijinga, “ Van Gaal aliiambia BBC Sport. 
Kwa upande mwingine Van Gaal alitokea kumtetea Marouanne Fellaini baada ya kiungo huyo kuonekana akimtemea mate Sergio Aguero.
“Televisheni ilimuonyesha akipiga kelele, na wakati mwingine ukipiga kelele unaweza kutokwa na mate kidogo” alisema kocha huyo lakini picha zinaonyesha Fellaini raia wa Ubelgiji akimtemea mate Aguero wakati akimlaumu kuwa alijiangusha.
Lakini picha zimebadili mchezo huo na huenda Mbelgiji huyo mwenye asili ya kiarabu akakumbana na adhabu ya FA.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top