Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MCHUNGAJI AKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA ZENYE THAMANI YA BIL 2 ZA KITANZANIA

dawaaa
Jeshi la Polisi kitengo cha Kupambana na Dawa za kulevya limekamata kilo40 za dawa za kulevya aina ya heroine zenye thamani ya shilingi bilioni2.

Tukio hilo lilitokea juzi eneo la Tegeta nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam ambapo Polisi walifaniikiwa kuwanasa watu wawili wakiwa na dawa hizo ndani ya nyumba inayomilikiwa na mchungaji ambaye wakati huo alikua katika kanisa lake lililopo eneo la Sinza.
Kamanda wa kikosi cha kupambana na dawa za Kulevya Godfrey Nzowa alilithibitishia Gazeti la MTANZANIA kuwa  kuwepo kwa tukio hilo akiomba jina la mchungaji huyo lihifadhiwe kuepusha kuvuruga uchunguzi.
“Ni kweli tukio la aina hiyo lipo  lakini watu kama hawa siwezi kusema moja kwa moja ni Mchungaji  ndio muhusika hadi nipate vithibitisho vya kutosha ikiwa kuendesha kanisa kwani wengi wao wanatumia makanisa kama mwamvuli wa kujificha na kufanya biashara hii,”Alisema Nzowa.
Alisema kwa sasa watu hao wanashikiliwa na Jeshi hilo ambapo wawili kati yao si raia wa hapa nchini wakati upelelezi ukiendelea kabla ya kuweka hadharani ukweli wa mambo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top