Chuo
kikuu cha Ruaha nchini Tanzania ni miongoni mwa vyuo vitatu vikuu
vilivyofeli katika mjadala wa kimataifa uliofanyika katika mahakama
maalum ya ICTR mjini Arusha.
Vyuo
vikuu vitatu vya Tanzania ambavyo vilishiriki katika mashindano ya
mjadala wa Afrika kuhusu Sheria za kimataifa za haki za kibinaadamu
yalioandaliwa na kamati ya kimataifa ya shirika la msalaba mwekundu ICRC
vimeshindwa kufika katika raundi ya mwisho.
Badala yake vyuo hivyo viliondolewa katika raundi za mapema ambapo mataifa manane ya Afrika yalishiriki.
ICRC imekuwa ikiandaa hafla kama hizo kwa kipindi cha miaka 14 sasa mjini Arusha.
Kulingana
na gazeti la the Citizen nchini Tanzania, vyuo vilivyoiwakilisha
Tanzania ni chuo cha kanisa katoliki cha Ruaha kutoka Iringa,Chuo cha
Iringa na Chuo kikuu cha Zanzibar.
Katika
raundi ya mwisho ya mashindano hayo yaliofanyika mwishoni mwa wiki
katika mahakama maalum ya kimataifa inayochunguza mauaji ya kimbari
nchini Rwanda ICTR mjini Arusha,chuo cha Strathmore University kutoka
Kenya kiliibuka mshindi na kufuatiwa na chuo cha Christian University
kutoka Uganda huku chuo cha Kunduyi pasi kutoka Zimbabwe kikiibuka
mshindi wa spika bora.
Raundi
ya mwisho ya mjadala huo ilisimamiwa na jaji wa mahakama hiyo Vagn
Joensen,jaji wa mahakama kuu ya Tanzania Stella Mugasha,jaji wa mahakama
ya haki katika Afrika mashariki Fanstin Ntezilyayo,John Joseph Wamwara
na Mutsa mangezi kutoka ICRC.
Judge
Joensen, ambaye alitoa zawadi kwa washindi aliyapongeza mashindano hayo
kama kifaa cha kuwahamasisha wanafunzi wa vyuo vikuu wanaofanya sheria
na kwamba itasaidia kuimarisha maono yao katika siku za usoni.BBC
SWAHILI
Post a Comment