
Basi
liitwalo Easy Bus lenye namba za usajili T 298 BLZ lililokuwa likitokea
Lilongwe Malawi likiwa katika mtaro wa Mlima Kitonga.



Foleni
kubwa iliyosababishwa na basi hilo baada ya kuingia mtaroni na kuziba
njia. Basi la abiria lenye namba za usajili T 298 BLZ likiwa linatolewa
katika mtaro wa Mlima Kitonga mapema leo baada ya kutumbukia. Hali hii
imesababisha foleni kubwa kwa magari huku mengine yakishindwa kuendelea
na safari zake. Kwa mujibu wa mashuhuda, chanzo cha gari hilo
kutumbukia mtaroni ni kufuatia kupata hitilafu na hatimaye uamuzi wa
kuliegesha kando ukafanyika kisha abiria wote wakashuka ili kusubiri
marekebisho hayo.
Haikupita
muda mrefu baada ya abiria kushuka gari lilikosa balansi, likaanza
kurudi kinyumenyume na kisha kuingia mtaroni. Hakuna mtu aliyefariki
dunia wala kujeruhiwa katika ajali hiyo.Credit Dj Sek Blog
Post a Comment