Mmoja
wa Watangazaji machachari wa Clouds FM,Adam Mchomvu akitoa muongozo
mfupi kwa baadhi ya Wafanyakazi wenzake waliomzunguka,kuhusiana na
ukataji na ulaji wa Ndafu kama ionekavyo pichani,wakati wa hafla ya
kutimiza miaka 15 ya kituo cha redio ya Clouds FM,tangu kuanzishwa kwake
nchini.Redio hiyo imejizolea umaarufu mkubwa Afrika Mashariki na Kati na Duniani kwa ujumla
Mkurugenzi
wa Uzalishaji na Vipindi Ruge Mutahaba akilishwa kipande cha Ndafu na
mtangazaji wa kipindi cha XXL,Dj Fetty,huku miluzi na shangwe za hapa na
pale zikiwa zimetawala mjengoni humo,Mikocheni jijini Dar
Msanii
mkongwe wa Muziki wa kizazi kipya,Prof Jay akilishwa kipande cha
ndafu,wakati wa hafla ya muendelezo wa redio hiyo kutimiza miaka 15
tangu kuanzishwa kwake nchini.
Mkuu
wa Vipidi wa Clouds FM,Sebastian Maganga akishukuru jambo kwa baadhi ya
Wafanyakazi wenzake mara baada ya kulishwa keki na Mtangazaji wa
kipindi cha XXL,Dj Fetty.
Dj
Mkongwe ndani ya Clouds FM,Dj Venture akilishwa keki kwenye hafla hiyo
ya kutimizwa miaka 15 kituo hicho maarufu cha redio hapa nchini na
kwingineko.
Mwanamuziki
mkongwe wa muziki wa kizazi kipya,Banana Zorro akihojiwa mambo kadhaa
kuhusiana na hafla ya muendelezo wa kituo hicho cha redio kutimiza miaka
15 tangu kuanzishwa kwake nchini.
Msanii wa zamani wa Bongofleva aliyewahi kuwa kwenye kundi la B Love M,Masiga Msigalla
Kulikuwepo na wimbo wa kuimba pamoja
Ndafu wa shughuli akiwa mezani
Ndafu akitolewa nje ili aliwe vizuri
Wadau mbalimbali pia walikuwepo.
Shayo akihakikisha kila mmoja anapata kipande cha Ndafu
Mkuu wa Vipindi wa Clouds FM,Sebastian Maganga akihojiwa machache na Mtangazaji wa Clouds TV,Antonia Nugaz
Kutoka Idara ya Muziki Clouds FM,anaitwa Othman Suka na Da Husna mtangazaji wa kipindi Leo Tena
Mrope nae akigawa vipande vya Ndafu
Kutabasamu,kuwhatsapika pia kulikwepo mjengoni hapa
''Heee hii imetoka vizuuuriiii..''
Adam
Mchovu akiwatangazia baadhi ya wafanyakazi wenzake kuhusiana na
utaraibu mzima wa kwenda kujiachia kwenye kiota cha maraha cha Escape
One.
Mazungumzo ya hapa na pale ya kishosti yalinoga pia huku ndafu akiliwa taratibuu.
Post a Comment