Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Arusha, imesema chama hicho hakina mgombea ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini, aliyeandaliwa hadi sasa.
Kimesema mgombea mwenye sifa za kulikomboa jimbo hilo, ambalo liko Chadema, hajajitokeza mpaka sasa.
Akizungumza
na Mpekuzi, Katibu wa CCM wa Wilaya ya Arusha ,Feruzi Banno alisema
chama kina utaratibu wake wa kampeni na chama hakina mgombea
aliyeandaliwa kwa kuwa muda wa kuandaa wagombea bado haujatangazwa.
Banno
alisema hayo alipotakiwa na mtandao huu, kufafanua kauli zilizozagaa
jijini Arusha kuwa chama hicho kimemwandaa mmoja wa wagombea ambaye
yuko mstari wa mbele kulitaka jimbo hilo kwa udi na uvumba na tayari
ameanza harakati za kampeni kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi wa
CCM kata, wilaya na mkoa.
Alisema taarifa hizo zimekuwa zikisambazwa na wana CCM wenye kutaka ubunge Jimbo la Arusha, ambao wanaoana kama wanatengwa.
Alisema
kura za maoni za kumsaka mgombea ubunge ndani ya chama, ndizo
zitakazoamua na si vinginevyo na kamwe chama hakitambeba mwana CCM .
Pamoja
na hayo yote, Katibu huyo alisema Jimbo la Arusha lenye asilimia kuwa
ya vijana, linahitaji mgombea mwenye kujichanganya katika rika zote na
anayekubalika bila ya kubabaisha, kwani huyo atafanya chama kufanya kazi
kwa urahisi na sio ngumu katika kampeni.
Banno
alisema kuwa CCM inahamu ya kulikomboa Jimbo la Arusha Mjini hivyo
hatuhitaji mgombea mzigo, ambaye itafika siku ya mwisho tukaanza
kulaumiana hilo halitakubalika kamwe kwa uongozi wa chama wilaya.
‘’Tunataka
mgombea kijana, mwenye kujichanganya katika vijiwe mbalimbali vya Jiji
la Arusha na mwenye kujulikana katika kila kona ya Jimbo la Arusha na
mgombea huyo bado hajajitokeza hadharani. Hiyo itasaidia chama kufanya
kazi ndogo sana lakina hatutaki mgombea ambaye chama kitafanya kazi ya
ziada kumnadi, hilo halitakubalika kamwe. ‘’
Baadhi
ya wana CCM waliojitokeza na kuonesha nia ya kuwania ubunge Jimbo la
Arusha Mjini ni Kamanda wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa
Arusha , Philemon Mollel na Wakili wa Kujitegemea, Victor Njau.
Mwingine ni Mjumbe wa Baraza Kuu la Vijana Taifa, Dk Arod Adamson na Deo Mtui.
Wengine
wanaotajwa kuwania kiti hicho ni wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM ya
wilaya ya Arusha, mjumbe wa NEC Arusha, God Mwalusamba, Mweka Hazina wa
Chama wilaya ya Arusha Victor Mollel, Katibu Mwenezi wa CCM wa wilaya
ya Arusha, Gasper Kishimbua na Halima Mamuya.
Baadhi
ya wagombea hao tayari wengine wameshaanza kuchapisha fulana na
kujitangaza kuwa ni wateuliwe wa chama, wenye lengo la kukomboa jimbo
hilo la Arusha Mjini, hatua inayopingwa na chama ngazi ya Wilaya.
Post a Comment