Moto mkubwa uliozuka eneo la Kibangu, Ubungo jijini Dar es Salaam umeteketeza viwanda vya kusaga plastiki, kuchomelea, useremala na kuunguza maduka mawili ya karibu pamoja na vibanda vingine vya biashara eneo hilo.
Watu walioshuhudia moto huo wamesema
moto ulianzia katika kiwanda cha plastiki na baadaye kusambaa maeneo
mengine huku wakilaumu kikosi cha zimamoto kuchelewa kufika eneo hilo
ambapo baada ya kufika walitaka kuwashambulia kwa mawe lakini Kikosi cha
Askari Polisi wakafanikiwa kudhibiti.
Eneo hilo linazungukwa na makazi ya watu pamoja na kanisa ambayo hayajaathirika na moto huo.
Post a Comment