Zile picha za mahaba zilizosambaa kwenye mitandao zikimuonyesha Staa wa Bongo Fleva,Ommy Dimpoz na Wema Sepetu wakiwa kitandani zimezidi kuzua utata baada ya Ommy kusema hakujua alipigwa saa ngapi kwani hakuwa na fahamu bali aulizwe Wema.
Ommy
akizungumza katika kipindi cha Uheard na Soudy Brown amesema kuwa
hana maelezo zaidi ya kuzungumza zaidi ya kusema kuwa hajui ni muda upi
zilipigwa picha hizo.
Wiki
hii picha hizo zilisambaa mitandaoni na kuzua maswali kuwa Ommy Dimpoz
ameamua kujiweka kwa Wema baada ya kuachana na aliyekuwa mpenzi wake
Diamond Platinum.
Hata hivyo, Aunty Ezekiel ambaye ni rafiki wa Wema amesema kuwa rafiki yake huyo alikwenda nchini Afrika Kusini kufanya video mpya ya ngoma ya Ommy.
Hata hivyo, Aunty Ezekiel ambaye ni rafiki wa Wema amesema kuwa rafiki yake huyo alikwenda nchini Afrika Kusini kufanya video mpya ya ngoma ya Ommy.
Wiki hii pia picha nyingine zilisambaa Wema akiwa na aliyekuwa mume wa Zari wakiponda raha nchini humo na kuzua sintofahamu.
Post a Comment