Katibu
Mtedaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Dk Charles Msonde ametangaza
matokeo ya mitihani ya Shule za Sekondari ya Kidato cha Nne ya mwaka
jana na kusema, kiwango cha ufaulu kimeongezeka kwa asilimia 10
ikilinganishwa na matokeo ya mwaka 2013.
Dk
Msonde amesema kuongezeka kwa kiwango cha ufaulu kutoka asilimia 58.25
hadi asilimia 68.33 kumetokana na mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (Big
Results Now - BRN).
Dk Msonde ameishukuru Serikali kwa BRN na Walimu kwa jitihada zilizofanikisha kupatikana kwa matokeo hayo.
Matokeo
haya yametolewa kwa kutumia mfumo mpya wa wastani wa pointi badala ya
madaraja kama ilivyozoeleka kwa miaka iliyotangulia.
Baraza
hilo limewafutia metokeo watahiniwa 128 wa kujigetemea kutoka vituo vya
Kisesa mkoani Mwanza na Lubabo huko Zanzibar kutokana na udanganyifu
uliokithiri.
Post a Comment