Habari
za uhakika kutoka chanzo chetu huko Mkoani Tanga, zinasema kuwa Askari
Polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi JWTZ, wamefanikiwa
kuwadhibiti watu wanaodaiwa kuwa ni miongoni mwa watu wanaounda kundi la
Al-shaabab waliokuwa wamejificha kwenye mapango ya Amboni huko mkoani
Tanga.
Aidha
imeelezwa kuwa taarifa ziliwafikia Polisi wa mkoa huo ambao nao pia
waliomba kuongezewa nguvu kutoka Jijini Dar es Salaam, jana majira ya
saa nane mchana ambapo Helkopta ya Polisi iliondoka jijini Dar ikiwa
imesheheni askari wenye zana kamili na kulizunguka Pango la Amboni na
kufanikiwa kuwashambulia.
Watu
hao walionekana kuwa wakaidi ambapo walianza kujibizana risasi na
askari Polisi hadi walipozidiwa na kuanza kutimua mbio wakielekea
mpakani mwa Nche ya Kenya, huku milio ya risasi ikisikika kutawala
mapangoni humo kwa muda mrefu hadi majira ya saa sita usiku wa jana.
Askari
wetu waliongeza nguvu kwa kuwashambulia kupitia anga kwa Helkopta huku,
Magari kadhaa ya Polisi nayo yakishambulia pembezoni mwa Mapango hayo
na kuwazidi nguvu ambapo hadi muda huu inasemekena kuwa bado askari wapo
eneo la tukio wakiendelea kuhakikisha usalama na kusafisha kabisa
harufu ya Al-Shaabab hao.
Imeelezwa
kuwa mwanzo wa Movie hili lilianza baada ya kukamatwa mtu mmoja
aliyehisiwa kuwa ni Al-Shaabab mkoani humo na baada ya kuteswa na
kusulubiwa aliamua kutaja kuwa hakuwa peke yake na kuwaongoza askari hao
hadi kwenye Mapango hayo na kuonyesha walipo wenzake, ambapo pia
alikiri kuwa ni miongoni mwa waratibu na waliowahi kufanya matukio
kadhaa ya uporaji wa silaha kwenye Vituo vya Polisi.
credit: Mafotoweb
Post a Comment