Beki ngangari wa kati wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, amejiondoa kwenye kikosi hicho kitakachoivaa Platinum ya Zimbabwe.
Timu hiyo, inatarajiwa kuvaana na Platinum katika mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika wikiendi hii kwenye Uwanja wa Taifa.
Cannavaro alisema amejiondoa kwenye kikosi hicho baada ya kupasuka juu ya jicho la kushoto na kusababisha ashonwe nyuzi saba.
Cannavaro
alisema, nyuzi hizo alishonwa juzi Jumatatu asubuhi kwenye Hospitali ya
Kilwa Road, Kurasini jijini Dar mara baada ya mechi hiyo kumalizika.
Aliongeza
kuwa, hataweza kucheza kutokana na maumivu makali anayoyasikia kwenye
jeraha hilo, hivyo ameona ni vyema akapumzika hadi jeraha hilo
litakapopona kabisa kwa hofu ya kujitonyesha.
“Ujue
nilitumia ujasiri sana kusimama na kuendelea kucheza mechi na Simba mara
baada ya kugongana na mchezaji wa Simba ambaye sijamjua ni nani na
nilidhani nimepasuka padogo kumbe ni pakubwa.
“Niligundua
nimepasuka pakubwa mara baada ya kwenda hospitali na kugundulika jeraha
ni kubwa na kutakiwa kushonwa nyuzi saba juu ya jicho langu,
nilinyanyuka kuendelea kucheza kutokana na mapenzi yangu na Yanga.
“Nilitamani
kucheza mechi na Platnum, lakini kutokana na jeraha hili kiukweli
sitaweza kucheza, nimeona nipumzike kwa kuhofia kujitonyesha, nyuzi saba
ni nyingi sana, yaani nina maumivu mara mbili ya kukosa fedha za ahadi
kama tukiifunga Simba na maumivu haya niliyoyapata,” alisema Cannavaro
kwa masikitiko makubwa
Post a Comment