ALIYEKUWA
mume wa mwanamitindo maarufu Bongo, Jacqueline Patrick, ambaye kwa sasa
yuko jela nchini China, Abdulatif Fundikira amesifu penzi analopata
kutoka kwa mkewe ambaye alikuwa Miss Tanzania 2010, Salha Israel.
Miss Tanzania 2010, Salha Israel siku ya ndoa yake.
Akizungumza
na gazeti hili hivi karibuni, kijana huyo maarufu kama Tiff, alisema
hajawahi kujua utamu wa ndoa kama sasa kwani mapenzi anayopata toka kwa
mkewe ni ya kiwango cha juu.
“Siwezi kukuficha, najisikia raha sana na ninaweza kusema naona raha ya ndoa hivi sasa na kamwe siwezi kujuta kumuoa Salha kwa kuwa ni mwanamke ambaye anajua kumjali mume, namshukuru sana Mungu kunipa mke ambaye ni wa maisha yangu,” alisema.

Post a Comment