Felix aliyasema hayo hivi juzi kati alipokuwa akifanya mahojiano na Global Tv online nakusababisha stori hii kuenea kwa kasi sana kwenye magazeti na blogs za udaku.
Leo kupitia ukurasa wake wa Instagram Wolper aliandika ujumbe unaoonyesha kwa namna moja au nyingine kitendo hicho amekichukulia kama ni changamoto tu za maisha ya zamani.
Wolper aliandika maneno haya kwa lugha ya kimombo
“The past can hurt but the way I see it, you can either run from it or learn from it”.
Kwa tafsiri isiyo rasmi anaamanisha kuwa mambo yaliyopita yanaweka kuumiza lakini kwa jinsi anavyo yatazama yeye , unaeza kuyakimbia au kujifunza kutokana yaliyopita.
Mara baada ya ujumbe huu, mashabiki wake wengi walimpa moyo huku wakimponda kijana Felix kwa kufanya kitendo ambacho wengi walisema cha kipumbavu.
Post a Comment